Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Julius Benedicto Mallaba enzi za uhai wake.
Mahakama ya Tanzania
inasikitika kutangaza kifo cha Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Julius Benedicto Mallaba kilichotokea
leo tarehe 19 Desemba, 2025, saa 10 alfajiri, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa sukari na shinikizo la
damu.
Marehemu Jaji Mallaba alizaliwa
tarehe 12 Machi, 1960. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe
25 Julai, 2015 na kustaafu rasmi mnamo tarehe 12 Machi, 2020.
Kwa Mujibu wa Msemaji wa
Familia, msiba upo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam. Taratibu nyingine
za mazishi zitatolewa na Familia.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki
kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA
LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni