- Wajadiliana juu ya utoaji wa elimu bora ya Sheria
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 15 Desemba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST), waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania Jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yamelenga kuhakikisha utoaji wa elimu bora ya sheria, upatikanaji wa mikopo na upatikanaji wa fursa kwa vijana kusoma Shule ya Sheria kwa vitendo.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akipokea nakala ya kitabu kutoka kwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samweli Maneno (kushoto). Kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Abdi Kagomba.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo wakati wa mazungumzo kati yake na Wajumbe wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo yaliyofanyika leo tarehe 15 Desemba, 2025 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo wakisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa wakati wa mazungumzo kati ya Wajumbe wa Taasisi hiyo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju yaliyofanyika leo tarehe 15 Desemba, 2025 kwenye Ofisi ya Jaji Mkuu jijini Dodoma.
(Picha na HABIBA MBARUKU & JEREMIA LUBANGO, Mahakama)






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni