Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju tarehe 15 Januari, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Viongozi hao
wamejadiliana kuhusu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na ushirikiano
kwenye masuala ya kisheria kati ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya China.
Yafuatayo ni
matukio katika picha ya mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,
Mhe. George Masaju na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian (kushoto) wakati Balozi huyo alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 15 Januari, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian (wa kwanza kulia kwa Jaji Mkuu) wakati Balozi huyo alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 15 Januari, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Wengine katika picha ni baadhi ya Viongozi wa Mahakama ya Tanzania (kulia) walioshiriki katika mazungumzo hayo.
Mazungumzo
yakiendelea kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju
(kulia) na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian wakati
Balozi huyo alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 15 Januari, 2026 ofisini kwake
Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimpatia Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian nakala za Jarida la Mahakama ya Tanzania (HAKI Bulletin) wakati Balozi huyo alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 15 Januari, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Viongozi kutoka upande wa Mahakama wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian (wa pili kushoto) wakati Balozi huyo alipomtembelea Jaji Mkuu tarehe 15 Januari, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Amidi wa Mahakama hiyo, Mhe. Augustine Mwarija, wa kwanza kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya na wa kwanza kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa China.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni