Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 22 Januari, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau wa Mahakama lengo likiwa ni kujadiliana juu ya uboreshaji wa utoaji wa huduma za Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.
Wadau walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Eliakim Maswi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Antony Sanga, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo, Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo na Wadau wengine.
Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Kwa upande wa Mahakama kikao hicho kimehudhuriwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. George Herbert, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri, Mhe. Desdery Kamugisha, Mkurugenzi wa Maktaba, Mhe. Kifungu Kariho na Maafisa wengine wa Mahakama.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kikao, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akiongoza kikao cha pamoja na Wadau wa Mahakama waliohudhuria katika kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu uliopo Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha pamoja na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu uliopo Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali pamoja na baadhi ya Viongozi na Maafisa wa Mahakama walioshiriki katika kikao hicho wakifuatilia kinachojiri katika kikao hicho.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Jaji Mkuu na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu uliopo Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Eliakim Maswi akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Jaji Mkuu na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Desdery Kamugisha akiwasilisha mada wakati wa kikao kati ya Jaji Mkuu na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo akizungumza jambo wakati wa kikao kati ya Jaji Mkuu na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Antony Sanga akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Jaji Mkuu na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao kati ya Jaji Mkuu na Wadau wa Mahakama kilichofanyika leo tarehe 22 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Antony Sanga.
Mdau kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni