Jumapili, 25 Januari 2026

TANZIA: JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU AFARIKI DUNIA


Mhe. Emilian Matata Ezekiel Mushi enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Emilian Matata Ezekiel Mushi, kilichotokea tarehe 24 Januari, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu Mushi aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe 7 Aprili, 1976 kama Hakimu Mkazi na kuhudumu katika vituo mbalimbali hadi tarehe 11 Juni, 2002 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na kuhudumu katika Kanda mbalimbali.

Enzi za uhai wake, Mhe. Mushi alihudumu pia katika nafasi ya Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto [IJA] kwa vipindi viwili tofauti, yaani mwaka 2000 hadi 2002, na mwaka 2004 hadi 2010 alipohamishwa kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo aliendelea na kazi mpaka mwaka 2012 alipostaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa tarehe 29 Januari, 2026 Kibaha Mwendapole, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mpendwa wetu

BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni