Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga amewaasa
wajumbe kuhusiana na suala la kuzingatia maadili kwa watumishi wote wa Mahakama
na kusema suala la maadili siyo la Mahakimu pekee bali linahusu watumishi wote
hata wasio Mahakimu.
Akifungua
kikao hicho cha menejimenti Mkoa wa Mbeya kilichofanyika tarehe 04 February,
2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mahakama Kuu Mbeya Mhe. Tiganga alisema “tuyaishi
maadili kwa kadiri kazi zetu zinavyotutaka kwa kuzingatia sheria na kanuni za kiutumishi
na si vinginevyo ili kujenga imani ya wananchi tunaowahudumia tunapokuwa kwenye
majukumu yetu ya kila siku,”
Aidha,
Mhe. Tiganga alisistiza kwamba, suala la maadili siyo kwa Mahakimu pekee ni kwa
watumishi wote hata watumishi wasio Mahakimu, nawasisitiza ninyi kama viongozi
nanyi mkawasisitize watumishi walio chini yenu kuzingatia maadili ya kiutumishi
ili kuboresha utendaji kazi wa Mahakama.
Mhe.
Tiganga aliongeza kuwa Mahakimu wote katika Vituo vyao kuweka mikakati imara ya
kumaliza mashauri kwa wakati na kuhakikisha kuwa wanamaliza kabisa mashauri ya
mlundikano mapema iwezekanavyo hasa katika Mahakama za mwanzo.
“Tuendelee
kuchapa kazi na tuongeze bidii kwenye usikilizaji wa mashauri na tuhakikishe
kuwa katika masijala zetu tumemaliza kabisa mashauri ya mrundikano,”alisema
Mhe. Tiganga
Vilevile,
kikao hicho kilitumika kujadili mapitio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Akiwasilisha taarifa hiyo Afisa Bajeti ambaye ni Afisa Rasilimali Watu Mahakama
Kuu Mbeya Bi. Sarah Lossi katika mapitio hayo ya bajeti alizungumzia kuhusu
hali ya rasilimali watu, fedha, hali ya majengo na hali ya bajeti ya Mwaka wa
fedha 2025/2026.
Aidha,
Bi. Sarah aliongeza kuwa, changamoto katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa
fedha 2025/2026 ni nyingi ambazo zinatakiwa kukabiliwa, mikakati na muelekeo wa
bajeti ya mwaka 2026/2027 ambapo alieleza juu ya majukumu na vipaumbele yaliyopangwa
kwa mwaka wa fedha 2026/2027
Kikao
hicho pia kilijadili taarifa ya utendaji kazi kwa robo ya pili ya mwaka
2025/2026 Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, katika taarifa iliyowasilishwa na Afisa
Utumishi Mahakama Kuu Mbeya Bw. Moses Luoga alitoa taarifa ya rasilimali watu,
usimamizi wa rasilimali fedha, hali ya mashauri, taarifa ya matumizi ya mifumo
ya TEHAMA, Utoaji wa elimu kwa umma na hali ya majengo mbalimbali ya Mahakama
mkoa wa Mbeya.
Vilevile,
kulitolewa mrejesho kuhusu taarifa za Mirathi kutoka katika kila Wilaya za Mkoa
wa Mbeya, Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama zote za Wilaya waliwasilisha taarifa
za mirathi kutoka katika Wilaya zao.
Akiwasilisha
taarifa za Mirathi Mjumbe kutoka Wilaya ya kyela Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama
ya Wilaya Kyela Mhe. James Mhanusi alisema kuwa, mikakati iliyowekwa ili
kupunguza na kumaliza kabisa bakaa ya fedha katika akaunti ya mirathi wilayani
Kyela.
“Tumefanya
jitihada kubwa kupambana na bakaa ya fedha ya mirathi katika Mahakama zetu kwa
kufanya vipindi redioni na tumepata fursa kwenye redio kufanya kipindi kimoja
kila wiki kutoa elimu kwa wananchi kuhusu elimu ya mirathi na kuwaomba wananchi
kufuatilia mirathi yao mahakamani,” alinukuliwa Mhe. Mhanusi
Aidha
kikao hicho pia kilijadili kuhusu taarifa ya upatikanaji na upimaji wa viwanja,
Pamoja na hatua iliyofikiwa katika kulinda mipaka ya Mahakama ili kufikia lengo
la Mahakama ya Tanzania lililokusudia kupeleka huduma ya Mahakama hadi kwenye
ngazi ya kata
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga
(Katikati) akiongoza kikao cha menejimenti Mkoa wa Mbeya, kulia ni Naibu
Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu na kushoto ni
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mervis Miti wakiwa kwenye kikao
hicho.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga
(Katikati) akiongoza kikao cha menejimenti Mkoa wa Mbeya, kulia ni Naibu
Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu na kushoto ni
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mervis Miti wakiwa kwenye kikao
hicho.
Sehemu
ya wajumbe katika kikao hicho
Mmoja
wa wajumbe akizungumza jambo katika kikao hicho (aliyesimama) Afisa utumishi
Mahakama ya Wilaya Mbeya Bi. Odilia Mapunda
Sehemu
ya wajumbe katika kikao hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni