Na. Fredrick Mahava- Mahakama, Sumbawanga
Watumishi
wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga wamepata mafunzo juu ya Maadili katika utumishi
wa Umma na mambo ya mchaka wa mtu mwenye uzoefu na maarifa kumsaidia mtu mwenye
uzoefu mdogo kwa kumpa ushauri, muongozo, maarifa na msaada ili akue kielimu,
kikazi au kimaisha (Mentorship) ambayo yalitolewa kwa njia mbili yaani uso kwa
uso kwa waliokuwepo ukumbini na kwa njia ya Mtandao kwa waliokuwa mbali.
Mafunzo
hayo yalifunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Sumbawanga Mhe. Fredrick Manyanda jana tarehe 06 Februari 2026 ambayo yalifanyika
katika Ukumbi wa Mahakama Kuu Sumbawanga.
Akizungumza
wakati anafungua mafunzo hayo Mhe. Manyanda alisema, Kanda ya Sumbawanga imejiwekea
utaratibu wa kufanya mafunzo kila Mwezi kwa watumishi ili kuwajengea uwezo na
kuwafanya kuwa wabunifu zaidi katika kazi zao za kila siku.
Mafunzo
hayo yalitolewa na wawezeshaji watatu ambao ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Sumbawanga
Mhe, Joseph Luambano, Afisa Utumishi Mwandamizi Mahakama Kuu Sumbawanga Bi.
Irene T. Mlangwa na Afisa Tawala Mahakama ya Hakimu Mkazi Rukwa Bi. Sarah C. Mwasomola
ambao wasifu wao ulisomwa na msimamizi wa Mafunzo hayo Mhe. Elisha Mwasomola.
Mada
ya Kwanza kuhusu Mentorship programu iliwasilishwa na Naibu Msajili Mahakama
Kuu Sumbawanga Mhe. Joseph Luambano ambaye aliwataka watumishi wote wenye
uzoefu wa kutosha kazini kuwa washauri (mentor) kwa wale ambao ndiyo
wameajiriwa na hawana uzoefu kazini. Pia alielezea kuhusu misingi ya Maadili
katika utumishi wa Umma na mambo ya mchaka wa mtu mwenye uzoefu na maarifa
kumsaidia mtu mwenye uzoefu mdogo kwa kumpa ushauri, muongozo, maarifa na
msaada ili akue kielimu, kikazi au kimaisha (Mentorship) kwa Maafisa wa
Mahakama kwamba njia za kufanya Mentorship na Miongozo mbalimbali ya kufanya
Mentorship.
Kwa
upande wake, wakilishi wa mada ya pili Afisa Utumishi Mwandamizi Mahakama Kuu
Sumbawanga Bi. Mlangwa na Afisa Tawala Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi
Rukwa Bi. Sarah ambao walifundisha kuhusu Maadili katika Utumishi wa Umma
walisema ni muhimu kuzingatia miongozo, kanuni na taratibu zote za utumishi wa
umma pale mtumishi unakuwa unamuhudumumia mwananchi ili kuondoa dukuduku la na
aweze kupata majibu sahihi ya shida yake.
Aidha,
Mhe. Manyanda wakati akichangi kuhusu mada zilizofundishwa alisema, suala la Mentorship
sio tu kutoka kwa mkubwa kwenda kwa mdogo bali pia linaweza kuwa kutoka kwa
mdogo kwenda kwa mkubwa.
Naye,
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Thadeo Mwenempazi alisema kwenye
suala ya Mentorship uhuru wa kujieleza unatakiwa kuwepo na utakuwa huru zaidi
kama unafanya mambo yako kwa usahihi na hapo ndipo suala la maadili
linapozingatiwa.
Wakati
wa mafunzo hayo watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga walipata wasaa wa
kuuliza maswali mbalimbali kuhusu mada zilizowasilishwa na kupewa majibu ambayo
yaliwasadia kuelewa zaidi.
Jaji
mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Fredrick
Manyanda akifungua mafunzo kwa watumishi wa Mahakama Kanda ya sumbawanga juu ya
Maadili katika utumishi wa Umma na Mentorship Programu
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Thadeo Mwenempazi akizungumza wakati
wa mafunzo hayo
Naibu
Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Joseph Luambano akiwasilisha Mada
wakati wa Mafunzo.
Sehemu ya Watumishi
wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa.
Afisa
Tawala Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Rukwa Bi. Sarah C. Mwasomola akiwasilisha
Mada wakati wa Mafunzo.
Afisa
Utumishi Mwandamizi Mahakama Kuu Sumbawanga Bi. Irene T. Mlangwa akiwasilisha
Mada wakati wa Mafunzo.
Mheshimiwa
Elisha Mwasomola akitoa mwongozo wa Mafunzo kwa Watumishi Kanda ya Sumbawanga
%20-%20Copy.jpg)
%20-%20Copy.jpg)
%20-%20Copy.jpg)
%20-%20Copy.jpg)
%20-%20Copy.jpg)
%20-%20Copy.jpg)
%20-%20Copy.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni