Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, akifungua mkutano wa Majaji
Wafawidhi wa Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe.Mohamed Chande Othman amewahimiza Majaji Wafawidhi wa Mahakama kuu ya
Tanzania kuhahakisha kuwa, mashauri yanamalizika kwa haraka katika kanda wanazozingoza.
Akifungua kikao cha Wahe.Majaji Wafawidhi wa kanda mbalimbali
za Mahakama Kuu ya Tanzania katika
ukumbi wa Mikutano cha Mwalimu Nyerere leo asubuhi, alisema kuwa lengo la kikao
ni kujadiliana kwa pamoja juu ya mgawanyo wa fedha za maendeleo zilizotolewa na
ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli. ‘’
Wahe. Majaji Wafawidhi kama mnavyo fahamu, Serikali imeipatia Mahakama fedha za
maendeleo Tsh Biloni 12.3 na sisi
lazima tuanishe mipango yetu ya maendeleo na kuona kuwa fedha hizo zinatumika
wapi na katika miradi ipi.
Tunamshukuru Mhe Rais kwa kutimiza ahadi yake, kama
mlivyosikia hotuba ya Mhe. Rais wakati maadhimisho ya siku ya Sheria alituomba
kuongeza kasi ya kumaliza mashauri na kupunguza mashauri kwa kasi kubwa.
‘’Nashukuru kuwa tumejitahidi vya kutosha kupunguza mashauri lakini bado lazima
tuongeze kasi, mfano kwa sasa ni 6% ya mashauri ndio yako zaidi ya miaka miwili ‘’ alisema
Jaji Mkuu. ‘’ Tulijiwekea malengo sisi kama Taasisi na hii imetusaidia sana’’
alisisitiza.
Mhe.Jaji Mkuu alisema kuwa pamoja na suala
la Bajeti ya Maendeleo iliyotolewa na Serikali, kikao kazi hicho kitajadili pia
masuala ya maadili ya Majaji na Mahakimu,mikakati ya kupambana na rushwa ,
mashauri ya uchaguzi, kupata taarifa ya utekelezaji wa kila kanda ya Mahakama
Kuu na kufanya tathmini ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano uliopita na
mikakati ya kumaliza mashauri ya muda mrefu.
Kuhusu Mahakimu 30-40 walioamua mashauri
chini ya 100, Mhe Jaji Mkuu alisema lazima wajieleze ni kwa nini waliamua
mashauri kama hayo na Tume ijiridhishe na utendaji wao wa kazi pamoja na
mazingira ya kazi.
Waheshimiwa
Majaji Wafawidhi walioshiriki katika Mkutano Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu,
wenye lengo la kutambua nafasi ya Majaji Wafawidhi katika kuboresha huduma za
Mahakama, jijini Dar es Salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (aliyeketi katikati), Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu, Mhe. Shaban Lila (kushoto), Jaji Mfawidhi Kanda ya
Dar es Salaam, Mhe. Moses Mzuna (kulia) katika picha ya pamoja na Majaji
Wafawidhi wa Mahakama Kuu mikoa mbalimbali.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (aliyeketi katikati), Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu, Mhe. Shaban Lila (kushoto), Jaji Mfawidhi Kanda ya Dar es
Salaam, Mhe. Moses Mzuna (kulia) katika picha ya pamoja Wasajili, Watendaji wa
Mahakama ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni