Jaji Mfawidhi Mahakama ya Kazi,
Mhe.Aisha Nyerere,(wa kwanza kushoto) akifungua rasmi mkutano wa wadau wa Mahakama ya Kazi (Kamati
ya Utatu) kuweza kukuchambua mafanikio na changamoto zinazoikabili mahakama ya
Kazi lengo ikiwa ni kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wakati katika mashauri
yanayowasilishwa mahakamani.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi na Walemavu, Mhe. Abdallah Possi, (aliyesimama), akizungumzia wajibu wa Mahakama ya Kazi katika kutambua changamoto na
mapungufu yaliyopo ili kuweza kuondokana na mlundikano wa kesi katika maswala
ya kazi.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Mhe. Nicholas Mgaya, (aliyesimama),mgeni rasmi katika kikao cha wadau wa Mahakama ya Kazi akisoma hotuba yake
kutathmini changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama na njia za kutatua
changamoto hizo ili kuweza kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati.
Mgeni Rasmi pamoja meza kuu
katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu, Watendaji na Wasajili wa
Mahakama ya Tanzania.
Wajumbe
wa Taasisi mbalimbali (ATE, TUCTA, LC, AG, TLS, CMA) walioshiriki katika
mkutano wa wadau wa Mahakama ya Kazi.
Mgeni
Rasmi pamoja meza kuu katika picha ya pamoja na Wadau wa Mahakama ya Kazi,
Wasajili wa mikoa mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania.
Mgeni Rasmi pamoja meza kuu katika picha ya pamoja na Wasajili, Watendaji na Watumishi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi
Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni