MAJAJI
WA MAHAKAMA YA JUU ‘SUPREME COURT’ CHINA WATEMBELEA MAHAKAMA YA TANZANIA
Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akisisitiza jambo alipokuwa na ugeni
wa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya juu ya China walipotembelea
ofisi za Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mhe. Zhang
Jiannan, Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu ya China, Kulia ni Mhe. Shaban Lila,
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Jaji Kiongozi wa Mahakama
ya Juu Nchini China Mheshimiwa Zhang Jiannan yuko Nchini kwa ziara ya kikazi yenye
lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi za Tanzania na
China.
Katika ziara yake Nchini,
Mheshimiwa Jiannan ambaye anamwakilisha Jaji Mkuu wa China, leo alikutana na
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman na
kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa Mahakama zao.
Akizungumzia changamoto za
Mahakama nchini China, Mheshimiwa Jiannan alisema hivi sasa Mahakama za China
zinakabiliwa na upungufu wa Majaji ikilinganishwa na idadi ya kesi
zinazosajiliwa.
Kwa Upande wake, Jaji Mkuu
wa Tanzania alisema baadhi ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania ni
pamoja na upungufu wa Mahakama za mwanzo.
Alisema ili kukabiliana na
upungufu huo, Tanzania inahitaji kuwa na Mahakama za Mwanzo 3000 nchi nzima.
Hivi sasa kuna Mahakama za Mwanzo karibu 960 nchini kote ambazo hazitoshi
ikilinganishwa na Idadi ya kata zilizopo Nchi mzima.Jaji Mkuu wa Tanzania
alimshukuru Jaji Mkuu Kiongozi wa China kwa kuitembelea Mahakama ya Tanzania.
Katika ziara yake nchini,
Jaji Jiannan ameongoza ujumbe wa Majaji na Watendaji wengine wa Mahakama wanne
kutoka nchini China.
Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akipokea zawadi kutoka kwa Mhe.
Zhang Jiannan, Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu ya China mara baada ya
mazungumzo baina ya pande mbili i.e Mahama ya Tanzania na Mahakama ya Juu ya
China.
Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (kulia), akimkabidhi zawadi ya sanamu ya
asili kwa Mhe. Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu ya China alipotembelea katika
Ofisi za Mahakama ya Rufani. Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano na
ushirikiano uliopo baina ya nchi za Tanzania na China.
Mhe.
Shaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania akiteta jambo na Mhe.
Zhang Jiannan, Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu ya China, ofisi kwake kwa Mhe.
Jaji Kiongozi, ugeni huo wa China ulipata nafasi pia ya kutembelea Mahakama Kuu
ya Tanzania ambapo walipata fursa ya kuelezwa mambo kadhaa juu ya utendaji kazi
wa Mahakama hiyo.
Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, (katikati), Mhe. Zhang Jiannan,
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu ya China (wa pili kushoto), Mhe. Mbarouk
Mbarouk, Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) (wa kwanza kushoto), Mhe. Shaban Lila,
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania pamoja na Maafisa wengine wa Mahakama
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Juu ya
China walipotembelea Mahakama ya Rufani mapema leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni