Kwa mujibu wa Kifungu
na. 107(A) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
itakuwa Mahakama. Na kazi kubwa ya Mahakama kama mhimili ni kutafsiri sheria
zilizotungwa na Bunge. Kwa wananchi walio wengi, Mahakama ndio kimbilio la
walio wengi kwa ajili ya kupata haki.
Tangu kupitishwa kwa
Sheria Namba 4 ya mwaka 2011 kumekuwa na maboresho mengi katika Mhimili wa
Mahakama .Kwa muda mfupi kumekuwa na mkakati wa makusudi kabisa kufanya maboresho katika
huduma za Mahakama. Maboresho hayo yamelenga katika kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata huduma iliyo bora kwa kuhakikisha kuwa, miundombinu ya Mahakama
inaboreshwa na inaendelea kuboreshwa siku hadi siku, maboresho ya upatikanaji
wa vitendea kazi kama magari na kompyuta.
Mahakama imeimarisha
mfumo wa kupata takwimu za mashauri mbalimbali ya kimahakama. Kwa wadau walio
wengi wanathamini sana mabadiliko yanayoendelea ndani ya Mahakama ya Tanzania.
Kutokana na maboresho yanayoendelea
kumekuwa na magawanyo mzuri wa utendaji kazi na kwa makusudi kabisa kwa
Wahe.Majaji na Mahakama ya Tanzania wanapaswa kusikiliza kesi 220 kwa mwaka.
Kwa mfano Mahakimu Wakazi hutakiwa kumaliza mashauri 250 kwa mwaka na Mahakimu
wa Mahakama ya mwanzo hutakiwa kumaliza mashauri 260 kwa mwaka. Na Mahakimu wote hupimwa kwa kiwango hiki.
Ukitolea mfano wa
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa Mwezi Aprili jumla ya kesi
217 zilifunguliwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili jumla ya mashauri 104
yalisikilizwa na kutolewa maamuzi, Mahakama ya Wilaya Temeke ilisikilia na
kutolea maamuzi jumla ya mashauri 278 kwa mwezi Aprili tu.
Kwa upande wa Mahakama
Kuu, Kanda ya Tabora, mwanzoni mwa mwezi Aprili jumla ya kesi 102 zilifunguliwa
hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili jumla ya kesi 86 zilisikilizwa na
kutolewa maamuzi.
Hii ni mifano ya baadhi
ya Mahakama kati ya nyingi zinazoendelea kusikiliza na kutolea maamuzi kesi mbalimbali
zinazoletwa Mahakamani kwa kasi kubwa, hii ni kutokana ana nia ya dhati na ari
ya utendaji.
Mbali na kujitoa kwa
dhati, Mahakama pia ina mikakati mingine kadhaa yenye lengo la kuboresha huduma ya utoaji haki nchini,
mikakati hiyo ni pamoja na ushirikiano na wadau wa sheria lengo ili
kuwashirikisha nini hasa matarajio ya Mahakama.
Kuwachukulia hatua kali
ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi Mahakimu wanaongundulika kujihusisha na
vitendo vya rushwa; Katika hili Tume ya Utumishi wa Mahakama imekuwa ikifanya
uchunguzi dhidi ya Maafisa wa Mahakama wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na
pindi wanapojirisha hatua kali huchukuliwa.
Uanzishwaji wa Idara ya
Ukaguzi na Maadili, kwa mujibu wa Muundo mpya wa Mahakama, idara hii
ilianzishwa lengo likiwa ni kuwafuatilia kwa karibu Mahakimu juu ya utendaji
kazi wao, vilevile kusimamia maadili/nidhamu ya Mahakimu katika utendaji wao wa
kila siku.
Kwa
wadau walio wengi wanaridhishwa na utendaji wa kazi wa Mahakama kutokana na
maboresho yanayoendelea katika Mahakama ya Tanzania. Ni kweli kuwa Mahakama ya
Tanzania kwa nyakati tofauti ilifanya utafiti wa kujua namna gani wadau na
Wananchi waridhika na huduma za Mahakama. Asilimia 62 ya Wananchi waliohojiwa
walijibu kuwa, wanaridhika na huduma inayotolewa na Mahakama ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni