Jumapili, 3 Julai 2016

JAJI MSTAAFU,MHE, DAMIAN LUBUVA ASIFU BIDHAA ZA TANZANIA.



Jaji Mstaafu Damian  Lubuva akiangalia kikapu cha asili ya  Kitanzania wakati akitembelea Maonyesho ya 40  Biashara ya Kimataifa yajulikanayo kwa jina la sabasaba katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dares Salaam .


Jaji Mstaafu Damian,Mhe.  Lubuva amesema Tanzania imepiga hatua katika kuboresha bidhaa zinazozalishwa  hapa nchini, hivyo inaweza kushindana  na bidhaa za nje.
Hayo yamesemwa na Jaji  Mstaafu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC),Mhe.  Lubuva,  wakati alipotembelea katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam kwenye Banda la NEC lililopo ukumbi  wa Jakaya Kikwete.
Jaji Lubuva alisema hayo wakati akifanya mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Banda la Jakaya Kiwete, Pride Tanzania, Mfuko  wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahakama ya Tanzania,  na Jeshi la Kujenga Taifa.
“ Bei za bidhaa zetu ni za gharama nafuu , sasa tujiendeleze kwa kuwa  viwanda kama Serikali ya Awamu ya Tano inavyosisitiza, tunaweza kushindana  na bidhaa za nje,alisema,”Mhe. Jaji Lubuva.
Akizungumzia kuhusu ziara yake katika maonyesho hayo, alisema  ametembelea ili aweze kujifunza baadhi ya mambo muhimu.


Jaji Mstaafu,Mhe. Damian  Lubuva akiangalia kibuyu cha asili ya  Kitanzania wakati akitembelea Maonyesho ya  40 ya Biashara ya Kimataifa yajulikanayo kwa jina la sabasaba katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.Kulia ni Meneja wa Pride Tanzania, Ruth Urassa Kanda ya Pwani.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni