Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (mwenye tai nyekundu) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Benki ya Dunia uliotembelea Mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo/Wilaya Kigamboni, (aliyepo katikati mwenye suti ya kijivu) ni Bw. Jim Brumby, 'Director of Governance' World Bank, Washington D.C, (wa pili kutoka kulia) ni Bw. George Larbi, Mwakillishi kutoka Benki ya Dunia, (wa kwanza kushoto) ni Bw. Denis Biseko, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, Ofisi ya Tanzania.
Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia ulitembelea Mahakama lengo likiwa ni kuangalia maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Mahakama ambapo sehemu ya fedha zake zitatoka Benki hiyo ya Dunia.
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kushoto) akiwa pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia uliotembelea katika jengo la Mahakama ya Kigamboni lililopo katika ujenzi, jengo hilo linajengwa kwa kutumia teknoloji ya Moladi, wa kwanza kulia ni Meneja wa Moladi-Tanzania.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo/Wilaya Kigamboni lililopo katika ujenzi chini ya teknolojia ya Moladi Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni