Hivi karibuni Maafisa wa ngazi mbalimbali za Mahakama nchini walikuwa na kazi ya kutoa elimu kwa watumishi kuhusiana na Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.
Katika kazi hiyo maalum iliyolenga kuwapa ufahamu watumishi juu ya Mkakati huo, Maafisa hao pia walipata wasaa wa kugawa vifaa kadhaa ikiwa ni pamoja na mabango yenye namba za simu za kila mkoa ili kuwawezesha wananchi kutoa taarifa ya vitendo vya ukiukaji wa maadili hususani vitendo vya rushwa vinavyofanywa na miongoni mwa Watumishi wa Mahakama. Mabango hayo na vifaa vingine vilitolewa katika Mahakama zote nchini pamoja na Ofisi za Wakuu wa Mikoa lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wananchi kutoa malalamiko yao pamoja na maoni ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionesha wananchi wakisoma mabango hayo yenye ujumbe maalum kuhusiana na rushwa na namba za simu za kila mkoa:
Baadhi ya wananchi wakiangalia bango katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara.
Baadhi ya wananchi wakiangalia bango lenye ujumbe wa kudhibiti vitendo vya simu ukiwa pamoja na namba za simu za mikoa mbalimbali wakilitazama bango hilo katika Mahakama ya Mwanzo Nkololo mkoani Simiyu.
Wananchi wakiangalia bango katika Mahakma ya Mwanzo Dutwa mkoani Simiyu.
Mahakama ya Mwanzo Somanda, Simiyu.
Wananchi wakiangalia bango lenye tangazo, Mahakama ya Wilaya Maswa.
Wananchi wa Wilayani Bariadi wakiangalia tangazo katika Mahakama hiyo ya Wilaya.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Urambo wakisoma bango lenye ujumbe maalum wa kupambana na rushwa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya.
Wananchi wa Urambo wakiendelea kusoma ujumbe maalum wa mapambano dhidi ya rushwa.
Baadhi ya Wananchi wa moani Iringa wakisoma bango katika Mahakama ya Mwanzo Bomani iliyopo katikati ya mji wa Iringa.
Mwananchi akisoma tangazo hilo Mahakama ya Wilaya Nzega.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni