Jumanne, 18 Oktoba 2016

JAJI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI HAKI KIMATAIFA JIJINI ARUSHA


 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifungua Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha. Mkutano huo umeandaliwa na Africa Group for Justice and Accountability.  

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability na aliyekuwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Mheshimiwa Hassan Bubacar Jallow kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha.  


Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Hayupo Pichani) wakati akifungua mkutano huo leo jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability Mheshimiwa Catherine Samba-Panza. 

 Mjumbe wa Taasisi ya Africa Group for Justice and Accountability ambaye pia ni Mkurugenzi wa WAYAMO Foundation, kutoka Berlin bibi Bettina Ambach akitoa neno la Utangulizi kabla ya Ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa leo jijini Arusha.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (katikati) akishiriki kwenye mjadala wakati wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha. 


Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye Majadiliano leo jijini Arusha. Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wamewakilisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini, Sierra Leone, Uganda, Tanzania, Kenya, na Botswana.    

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni