Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali amewataka Majaji wa
Mahakama Kuu nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia Maadili, kuwa waaaminifu na
kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kesi zimalizike kwa haraka katika Mahakama
mbalimbali.
Akifungua Mafunzo ya siku
tano ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tazania kuhusu Uongozi katika shughuli za
Mahakama leo jijini Arusha, Jaji Kiongozi
amesema lengo la Mafunzo hayo ni kujadiliana kwa kina nini kifanyike ili kesi
zimalizike mapema kwenye mahakama mbalimbali nchini.
Jaji Wambali alisema katika mkutano huo, Majaji watapata
nafasi ya kujifunza Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania
wenye nguzo tatu ambazo ni pamoja na masuala ya Utawala, Upatikanaji wa haki
kwa wakati na imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika
shughuli za Mahakama.
Katika Mafunzo hayo pia
Majaji watajadiliana ni nini kilifanyika mwaka jana katika umalizwaji wa
mashauri, changamoto zilizojitokeza na nini kifanyike ili kutatua changamoto
zinazojitokeza katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.
Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akifungua Mafunzo ya Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania katika Ukumbi wa AICC leo jijini Arusha. Mahakama
inaendesha Mafunzo kwa Majaji wote wa Tanzania ambapo Majaji wa Mahakama ya Rufani
wanahudhuria Mafunzo kuhusu namna ya kutoa maamuzi ya Mahakama katika
usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, Majaji Wafawidhi kuhusu Usimamizi wa
uendeshaji wa kesi wakati Majaji wengine wanapatiwa mafunzo kuhusu uongozi na
usimamizi wa kuleta mabadiliko.
Naye
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati
akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo alisema yamegawanyika katika makundi matatu ambapo
kundi la kwanza ni la Majaji wa Mahakama ya Rufani, kundi la pili ni la Majaji Wafawidhi wa Kanda 14 za Mahakama Kuu ya Tanzania na kundi la Tatu ni la Majaji wengine wote.
Alisema Majai wa
Mahakama ya Rufani watapatiwa Mafunzo kuhusu namna ya kutoa maamuzi ya Mahakama
katika usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, ambapo Majaji Wafawidhi watapewa
mafunzo kuhusu Usimamizi wa uendeshaji wa kesi wakati Majaji wengine watapatiwa
mafunzo kuhusu uongozi na usimamizi wa kuleta mabadiliko.
Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa
na Benki ya Dunia ni Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama
ya Tanzania na yanalenga katika kuboresha utendaji kazi na kuleta mabadiliko
ndani ya Mahakama.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Juma (wa pili kushoto) akiwasili katika ukumbi wa AICC jijini Arusha kuhudhuria
Mafunzo ya Majaji yaliyoanza leo. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Juma (wa pili kushoto) akiwasili katika ukumbi wa AICC jijini Arusha kuhudhuria
Mafunzo ya Majaji yaliyoanza leo. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali. Kushoto kwa Jaji Mkuu ni
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati na kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama Bibi Wanyenda Kutta.
Waheshimuiwa Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye ufunguzi wa Mafunzo yao yaliyoanza leo
jijini Arusha.
Baadhi ya Waheshimuiwa
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye ufunguzi wa Mafunzo yao
yaliyoanza leo jijini Arusha. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda
ya Mbeya Mhe. Noel Chocha, kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni
ya Kazi Mhe. Aisha Nyerere na kulia ni Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Mwanza Mhe.
Robert Makaramba.
Waheshimuiwa Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye ufunguzi wa Mafunzo yao yaliyoanza leo
jijini Arusha.
Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma(waliokaaa -katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani mara baada ya ufunguzi wa
Mafunzo yao leo jijini Arusha.
Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma(waliokaaa -katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Waheshimiwa Wasajili na wanasheria wa Mahakama Mahakama ya Rufani mara baada ya ufunguzi wa
Mafunzo ya Majaji leo jijini Arusha.
Waheshimuiwa Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mafunzo yao yaliyoanza leo
jijini Arusha.
Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mara baada ya kufungua Mafunzo yao leo katika Ukumbi wa AICC leo jijini Arusha.
Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma(kushoto) akiwa katika katika Mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Mahakama ya Rufani kuhusu namna ya kutoa Maamuzi ya Mahakama katika
usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, yaliyoanza leo jijini Arusha.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye Mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Mahakama ya Rufani kuhusu namna ya kutoa Maamuzi ya Mahakama katika
usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, yaliyoanza leo jijini Arusha. Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati akiwa kwenye Mafunzo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani leo jijini Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni