Hakimu Mkazi Mwandamizi
Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa-Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele akifunga rasmi
mafunzo ya siku tano ya Uandishi wa Habari za Mahakama yaliyotolewa kwa
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mhariri wa gazeti la
Mtanzania, Bw. Bakari Kimwanga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Waandishi
wa Habari na Wahariri walioshiriki katika Mafunzo hayo, katika maneno yake ya
shukrani Bw. Kimwanga ameishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kuandaa mafunzo hayo
kwani wamejifunza mambo mengi ya Kimahakama ambayo yatawasaidia kama mwongozo
katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.
Mwandishi kutoka gazeti
la Daily News Bw. Faustine Kapama (kushoto) akipokea cheti cha ushiriki wa
Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Mahakama kutoka kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi
Mfawidhi, Mhe. Elizabeth Nyembele, jumla Washiriki 30 walitunukiwa vyeti hivyo.
Aliyesimama kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama
ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe, kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Kitengo cha Maboresho
Mahakama ‘JDU’, Dkt. Cosmas Mwaisobwa.
Mwandishi wa Habari
kutoka ‘Channel Ten’, Bw. Fred Mwanjala akipokea cheti.
Mwandishi kutoka ITV,
Bi. Futuna Suleiman akipokea cheti chake.
Mgeni rasmi (katikati)
pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki katika Mafunzo ya siku tano (5) ya
uandishi wa Habari za Mahakama.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Wanahabari huku wakifurahia vyeti vyao walivyotunukiwa baada ya kumaliza rasmi mafunzo ya Uandishi wa habari za Mahakama.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro yalifungwa rasmi Julai 20, 2018.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro yalifungwa rasmi Julai 20, 2018.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni