Waandishi wa habari za Mahakama wamefanya
mafunzo kwa vitendo katika Mahakama za Mkoa wa Morogoro ili kuona namna
Mahakama hizo zinavyotekeleza majukumu yake ya kila siku.
Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wadau wa
mahakama wakiwemo waandishi wa habari wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi
kwa weledi.
Akitoa maelekezo namna mahakama zinavyofanya
kazi, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe.
Elizabeth Nyembele amesema kuwa , katika mahakama zipo kesi zinazosikilizwa
katika Mahakama za wazi na nyingine husikilizwa Mahakama za ndani( Chamber).
” Kesi zote zinazohusu unyanyasaji wa
kijinsia mfano ubakaji, kesi za mambo ya ndoa au kesi yoyote ambayo itamhusisha
mtoto kesi zao husikilizwa katika mahakama za ndani (Chamber)” ameongeza Mhe.
Hakimu Nyembele.
Aidha, Mhe. Hakimu Nyembele amesema kuwa kwa
mkoa wa Morogoro wamekuwa wakipokea kesi nyingi zinazohusiana na masuala ya
unyang’anyi, madawa ya kulevya na ujangili unaosababishwa na mkoa huo
kuzungukwa na mapori.
Akizungumza kuhusu suala la rushwa kwa
makarani wa mahakama, Mhe. Nyembele ametoa rai kwa watumishi wote wa mahakama
kuepuka kupokea rushwa na kuwa waaminifu katika utendaji wao.
Vilevile amesema kuwa katika kudhibiti suala
la rushwa katika mahakama nchini, mahakama imetoa elimu kwa umma pamoja na
matangazo ya huduma mbalimbali za kimahakama zinazotolewa bure mfano nakala za
hukumu.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Agnes Ringo amesema kuwa kwa sasa
kuna utaratibu mpya wa namna kesi za watoto zinavyoendeshwa bila kutoa
utambulisho rasmi wa mtoto husika.
Nae Mtendaji Mkoa wa Mahakama Nestory
Mjunangoma amesema kuwa katika mkakati wa kuboresha huduma za mahakama,
Mahakama mkoa wa Morogoro inatarajia kuanza ujenzi wa ghorofa nne katika mwaka
huu wa fedha zitakazokuwa na huduma zote za kimahakama kuanzia Mahakama ya
Mwazo hadi Mahakama Kuu.
Aidha, Mjunangoma ameongeza kuwa ujenzi huo
unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Mafunzo hayo ni moja ya mradi wa maboresho ya
huduma za mahakama inayotekeleza programu mbalimbali chini ya mpango mkakati wa
mahakama wa miaka mitano 2015/2016-2019/202 iliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi
wa Mahakama chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
Hakimu Mkazi
Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele
akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotembelea katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Morogoro kwenye moja ya ziara za kimafunzo wakiwa katika semina ya
Waandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro.
Waandishi wa
Habari waliotembelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro wakimsikiliza Hakimu
Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Mhe. Elizabeth Nyembele (hayupo pichani) alipokuwa
akiwapa ufafanuzi juu ya matumizi ya Mahakama ya wazi ‘open court’
Mwandishi
kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Bw. Alpha Wawa akiuliza jambo kwa
Mhe. Nyembele.
Mtendaji wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Bw. Nestory Mujunangoma akifafanua jambo kwa
Waandishi wa Habari waliotembelea katika Mahakama hiyo.
Hakimu Mkazi
Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele
akiendelea kutoa somo kwa waandishi wa habari waliopo katika semina ya
uandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro, lengo la ziara hiyo ni
kujifunza kwa vitendo jinsi Mahakama inavyofanya kazi.
Waandishi wa
Habari waliotembelea Mahakama ya Mkoa Morogoro wakisoma tangazo linaloonesha
dalili za Rushwa lililobandikwa katika Mahakama hiyo, lengo la Matangazo hayo
ambayo yamebandikwa katika Mahakam azote nchini ni kuzuia na kutokomeza vitendo
vya rushwa Mahakamani.
Hakimu Mkazi
Mfawidhi-Mahakama ya Wilaya Morogoro, Mhe. Agnes Ringo (aliyesimama kulia)
akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari waliotembelea Mahakama hiyo mapema
Julai 19.
(Picha na
Mary Gwera, Mahakama-Morogoro)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni