Imeelezwa kuwa watu walio katika hatari ya kupata
maambukizi ya homa ya ini kwa urahisi ni watumiaji wa dawa za kulevya, watoto
wadogo na watoa huduma za afya, ambapo wamekuwa wakipewa kipaumbele kupata
chanjo ya ugonjwa huo dhidi ya maambukizi.
Hayo yamesemwa
na Daktari Bingwa wa Virusi vinavyosababisha Saratani, ambaye pia ni mtafiti
anayefanya tafiti za seli za saratani, Dkt. Kandali Samweli
wakati wa
uendeleaji wa zoezi la upimaji homa ya ini kwa hiari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mahakama Kuu ya
Tanzania.
Alisema kwaupande wa wanawake upimaji huo ni fursa
ya kuwakinga watoto, vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
Dkt. Samweli aliongeza kuwa kupata chanjo ya ugonjwa huo, sio kinga
dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa kuwa Virusi vya Hepatitis B hushambulia ini, wakati
VVU huathiri sehemu nyeupe za damu (RNA). Pia alisitiza kwamba watu wanaopata
chanjo hiyo, hawatakiwi kunywa pombe mara baada ya chanjo mpaka saa 24 kupita.
Hata hivyo kunaweza kuwa kuna mfanano wa dalili za
ugonjwa wa Ukimwi na ugonjwa wa ini, ambapo alizitaja dalili za ugonjwa wa homa ya ini ambazo ni ngozi na macho kuwa ya njano pamoja na kuwashwa ngozi, huku akifafanua kwamba dalilihizo hujitokeza mwishoni ambapo mgonjwa anakuwa ameathirika kwa muda mrefu.
“Hakikisheni mnatunza kadi mlizopatiwa wakati wa chanjo ili ziweze kuonyesha mlolongo mzuri wa utoaji wa chanjo hiyo, mpaka mtakapomaliza awamu zote tatu, zikiwemo taarifa zote za afya,” alisema Dkt. Samwel.
Upimaji huo, ulioanza jana ambao umehusisha baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam waliojitokeza kwa hiari, umemalizika leo Septemba 20, mwaka huu.
Naibu
Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Augustine Rwizile,
akichukuliwa kipimo kwa ajili ya kupima homa ya ini na Mtaalamu wa Maabara kutoka Tasisi ya Saratani Ocean Road, iliyopo jijini Dar es Salaam, Bw. Constatine Anga.
Baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakisubiri huduma ya upimaji homa ya ini katika ukumbi wa mikutano Mahakama Kuu ya Tanzania.
Daktari
Bingwa wa Virusi vinavyosababisha Saratani, ambaye pia ni mtafiti anayefanya
tafiti za seli za saratani, akitoa ufafanuzi juu ya kipeperushi chenye maelezo
kuhusu homa ya ini.
Askali Polisi ‘CPL’ wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Chrispine Alex. Akichukuliwa kipimo kwa ajili ya kupima homa ya ini. |
Mlinzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
Naima Mandai akichukuliwa kipimo kupima homa ya ini
Askari Magereza, Nicky Nyandura, wa Gereza la
Segerea akichukuliwa kipimo kwa ajili ya kupima homa ya ini.
(Picha na Aziza Muhali – (SJMC) |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni