Na Aziza Muhali. (SJMC)
Daktari Bingwa wa Virusi vinavyosababisha Saratani
ambaye pia ni mtafiti anayefanya tafiti za seli za saratani kutoka Taasisi ya
Saratani ‘Ocean Road’, jijini Dar es Salaam, Kandali Samweli, amewataka
watumishi wa Mahakama ya Tanzania kujitokeza
mapema kuchunguza afya zao na kupata chanjo dhidi ya maambukizi ya homa ya Ini ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.
mapema kuchunguza afya zao na kupata chanjo dhidi ya maambukizi ya homa ya Ini ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.
Wito huo umetolewa, leo Septemba 19, 2019 na Daktari
huyo wakati wa utoaji elimu, upimaji hiari na utoaji chanjo dhidi ya homa ya
Ini kwa watumishi hao, kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam, unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa
Mahakama Kuu, uliopo jijini Dar es Salaam, ambapo takribani watumishi
170 wanatarajiwa kufanyiwa kipimo cha ugonjwa huo kwa hiari.
Akizungumza na watumishi hao, mahakamani hapo, Dkt,
Samweli, amesema chanjo hiyo hutolewa kwa awamu tatu, ambapo ya kwanza hutolewa
mara baada ya kipimo cha Hepatitis B, ya pili hutolewa mwezi mmoja baada ya
chanjo ya kwanza, na chanjo ya tatu hutolewa miezi sita baada ya chanjo ya
kwanza.
Dkt. huyo alieleza kuwa katika makundi ya virusi vya
‘Hepatitis’ A, B, C na D homa ya ini husababishwa na kirusi aina ya ‘Hepatitis
B’. Hivyo tafiti zinaonyesha kwamba mtu mmoja kati ya ishirini anamaambukizi ya
‘Hepatitis B’.
Alifanunua kuwa chanjo hiyo ilianza kutolewa kwa watoto mnamo
mwaka 2002 ambapo chanjo hiyo huambatanishwa na chanjo nyingine zinazotolewa
punde mtoto anapozaliwa.
‘Chanjo hii ilianza kutolewa mwaka 2002 kwa watoto
na inaambatanishwa na chanjo nyingine kwenye kadi ya mtoto, hivyo wanaotakiwa
kupata chanjo hii ni waliozaliwa mwaka 2001 na miaka ya nyuma, na tayari tumeshaanza
kutoa chanjo hii kwa watu wengine.’ alisema Dkt. Samweli.
Alisema chanjo hiyo hutolewa kwa rika na jinsia
zote, na ni salama kwa wajawazito na wanawake wanaonyonyesha.
Alizungumzia kuhusu dalili za ugonjwa huo, alisema hazionekani kwa urahisi kwani hujitokeza baada
ya muathirika kuathirika kwa muda mrefu.
Alizitaja
baadhi ya njia zinazoweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo, kuwa ni kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto
wakati wa kujifungua, mgusano baina ya mtu na mtu kupitia damu na majimaji
mengine ya mwili, ngono zembe, kuchangia vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye virusi
hivyo na kuongezewa damu iliyoathiriwa
na virusi hivyo.
Aidha jamii
inatakiwa kuchunguza afya zao kwa kupata kipimo hicho, ikiwemo chanjo
mapema kwani mtu anaweza kupata virusi hivyo bila dalili kujitokeza, kwani dalili
zinajitokeza baada ya madhara makubwa,’ alisisitiza huku akisema athari za kuishi na virusi vya Hepatitis B
pasipo tiba huweza kusababisha Saratani ya Ini.
Kwa upande
wake Naibu Msajili Mahakama Kuu, Mhe. Devotha Kamuzora, amesema kuwa huduma
hiyo ya utoaji chanjo dhidi ya homa ya ini ni nzuri na imerahisishwa kwa
kuletwa karibu yao kwani imewasaidia watumishi kujua hali zao juu ya ugonjwa huo, pia kuchukua tahadahari dhidi ya
maambukizi.
Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) akipatiwa elimu
kuhusu upimaji wa ugonjwa wa homa ya ini leo na Daktari Bingwa vya Virusi vya Saratani, Kandali Samweli (wa pili kulia)
kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam wakati wa
kampeni ya upimaji wa hiari wa ugonjwa huo unaofanyika kwa Watumishi wa
Mahakama Kuu na Mahakama Kuu Kanda ya
Dar es Salaam, ambapo unaofanyika kwa
muda wa siku tatu katika ukumbi wa Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam.
Mtendaji wa Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Gaston Kanyairita (kulia) akimsikiliza
Daktari Bingwa vya Virus vya Saratani, Kandali Samweli (wa pili kulia) kutoka
Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam wakati akitoa elimu wa upimaji wa hiari wa homa ya ini unaofanyika kwa Watumishi wa Mahakama Kuu na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, (katikati)
ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Peter Machalo,
(aliyesimama)ni Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Wilbert Chuma.
Daktari Bingwa vya Virusi vya Saratani, Kandali Samweli (katikati) kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam, amkipatia elimu kuhusu upimaji wa homa ya ini Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.Leila Mgonya, (wa pili kulia)n wakati wa uhamasishaji wa upimaji wa hiari wa ugonjwa huo unaofanyika kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu.Kulia wa kwanza ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Lucy Tungaraza na kushoto wa kwanza Muuguzi, Bi. Odilia Masawe na Mtaalam wa Maabara, Bw. Costantine Anga wote wanatoka katika taasisi hiyo.
Afisa TEHAMA wa
Mahakama Kuu, Bi. Mwanaisha Mkweya akifanyiwa kipimo cha ugonjwa wa homa ya ini
na Mtaalamu wa Maabara kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Bw. Constantine
Anga.
|
Afisa Utumishi
Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Bw. Kenedy Nsenga akifanyiwa kipimo cha ugonjwa wa
homa ya ini na Mtaalamu wa Maabara kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Bw.
Constantine Anga.
|
Naibu Msajili wa
Mahakama Kuu, Mhe. Devotha Kamuzora (wa pili kushoto) akijiandikisha kwa ajili
ya upimaji wa ugonjwa wa homa ya ini. Kushoto wa kwanza ni Naibu Msajili wa
Mahakama Kuu, Mhe. Nyigulila Mwasoba. Kulia ni Mfamasia kutoka Taasisi ya
Saratani Ocean Road, iliyopo jijini Dar es Salaam, Bw. Joseph Ryoba.
(Picha na Magreth
Kinabo)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni