Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka wahitimu wa Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) kutumia silaha ya elimu ya sheria kuitumikia jamii
kikamilifu.
Aidha,
Jaji Mkuu amesema kwamba wahitimu hao wanapaswa kuinoa elimu hiyo kila wakati
ili silaha hiyo iwe na nguvu ya kuibadilisha dunia.
Prof.
Juma alisema hayo katika sherehe za mahafali ya 19 ya Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto (IJA) kwa wahitimu wa Stashada na Astashahada ya Sheria,
yaliyofanyika leo Novemba 29, mwaka huu chuoni hapo, wilayani Lushoto mkoani
Tanga.
‘Katika fani ya sheria, moja ya njia ya kuinoa
silaha hiyo ni kujisomea kila wakati kwa sababu sheria na kanuni huwa
zinabadilika mara kwa mara. Sio vyeti vyenu vitakavyofanya kazi ya kutoa
huduma. Kwa kuhitimu hivi leo haina maana kwamba mtakuwa mmemaliza kujifunza
masuala yote ya kisheria.
‘Bali
mnapaswa kuendelea kuwa wanafunzi kila wakati ili kujua sheria mpya na kanuni
zake pindi zinapobadilika. Mhitimu mzuri ni yule anayeacha milango wazi ya
kujifunza kutoka kwa wengine’.alisema Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu aliwaasa wahitimu hao, popote pale
watakapokuwa kujifunza jambo jipya kila siku ili wasipitwe na wakati ili kutoiaibisha
fani yao, hivyo wajiendeleze hadi
kufikia viwango vya juu kabisa katika fani hiyo muhimu.
‘Jengeni tabia ya kujisomea wenyewe vitabu ili
kuendelea kujielimisha. Kamwe usimtegemee mtu mwingine asome kisha akuelekeze.
Katika kujisomea, hakikisheni mnasoma pia mambo yasiyo ya kisheria kwa mfano
hivi karibuni, Mhe. Benjamin William Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu)
alizindua kitabu chake “My Life” My Purpose, A TANZANIA PRESIDENT REMBERS”,’
alisisitiza.
Alisema
kitabu hicho kitawaongezea ufahamu wa historia ya nchi yetu
kupitia miaka 81 ya maisha ya Rais huyo wa Awamu ya Tatu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho, lililomaliza muda
wake, Mhe.Jaji Dkt. Gerald Ndika, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani
Tanzania, alisema mahafali haya ya 19, yamefanya jumla ya wahitimu 6,037 katika
ngazi ya Stashahada na Astashada ya Sheria tangu kilipoanzishwa mwaka 2001.
Naye
Mkuu wa chuo hicho, Mhe Jaji Dkt.Paul
Kihwelo alizitaja takwimu za wahitimu hao
kwa mwaka huu, kwa upande wa Stashahada ya Sheria kati ya wahitimu 169 wanaume ni 93 (55.03%) na wanawake 76 (44.97%)
na kwa upande wa Astashahada ya Sheria, kati ya wahitimu 234 wanaume ni 102
(43.59%) na wanawake ni 132 (56.41%).
Mahafali hayo yalihudhuriwa na viongozi
mbalimbali, pia baadhi wahitimu walizawadiwa vyetieti, vitabu pamoja na fedha
taslimu kutoka chuo hicho na Mahakama
yaTanzania.
Pia
wahitimu bora wawili kutoka kutoka ngazi hizo, waliopata wastani wa daraja ‘A’ katika
somo la mwenendo wa mashauri ya madai na
jinai walipewa zawadi kutoka kwa Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma(aliyevaa kofia
nyekundu) akiwa katika maandamano ya
mahafali ya 19 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).Wengine ni baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho na viongozi
wengine. Maandamano hayo yamefanyika
leo, Novemba 29, mwaka huu.
Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wa ngazi ya
Astashahada ya Sheria wakiwa katika
mahafali hayo.
|
Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto (IJA) wa ngazi Stashahada ya
Sheria wakiwa katika mahafali hayo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amkipatia zawadi mhitimu bora wa ngazi Astashahada ya Sheria, Saida Rajabu aliyepata wastani wa daraja ‘A’ katika somo la mwenendo wa mashauri ya madai na jinai hizo.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw.
Mathias Kabunduguru (kulia wa tatu) akizungumza jambo na Balozi Mteule, Mhe.
Hussein Kattanga (kulia wa nne).
|
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim
Hamis Juma, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa
Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, waliomaliza muda wao.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wa ngazi Stashahada ya Sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wa ngazi Astashahada ya Sheria.
(Picha na Magreth Kinabo na Ibrahim Mdachi-Lushoto).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni