Na Festo Sanga- Mahakama Kuu Kigoma
Wajumbe kutoka Benki ya Dunia
wamekagua jengo jipya la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma ili kuona ufanisi wa
mfumo wa haki Jumuishi (intergrated Justice center) ambapo wamepongeza namna Mahakama
hiyo ilivyojipambanua kuwahudumia wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara
ya kukagua jengo hilo, Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia Bwn. Walid Malik amesema
kufuatia hatua hiyo nzuri ya Mahakama Kuu ya Kigoma wananchi sasa wataanza kufika
Mahakamani hapo kujifunza namna huduma inavyotolewa.
Akizungumza katika kikao cha
pamoja kati ya Watumishi wa Mahakama na wajumbe wa Benki ya Dunia, Jaji Mfawidhi
wa Mahakama kuu kanda ya kigoma Mhe. Ilvin Mugeta alisema jengo hilo limeanza
kutoa huduma rasmi Disemba 10, mwaka jana ambapo alisema ushirikiano wa wadau
waliopo katika Jengo hilo pamoja na mikakati waliyojiwekea vimechangia kusukuma
mashauri ya madai na jinai kumalizika kwa wakati.
Kwa upande wake, Naibu
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Mheshimiwa Arnold Kirekiano alieleza kuwa
asilimia themanini na tano (85%) ya mashauri yaliyomalizika hadi January 31,
2020 yalishughulikuwa ndani ya miezi minne, jambo lililopelekea kanda hiyo kuweka mkakati wa kupunguza
muda wa mashauri mahakamani.
Naye Mwenyekiti wa Mawakili Mkoa
wa kigoma Bw. Ignatus Kagashe ameishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kujenga
jengo hilo ambalo ni wezeshi kimiundombinu na linalotoa fursa za ofisi kwa
wadau mbalimbali.
Alisema uanzishwaji wa
Mahakama Kuu kanda ya kigoma umewapunguzia gharama wananchi wa Mkoa wa Kigoma
ambao awali walikuwa wakipata huduma za Mahakama Kuu Mkoani Tabora.
Wajumbe kutoka Benki ya Dunia
wamewasili nchini kwa ajili ya kufanya tathmini ya maboresho yanayofanywa na
Mahakama ya Tanzania kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa majengo ya
Mahakama.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Mhe. Ilvin Mugeta (katikati) akifafanua
jambo wakati wa kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika mwishoni
mwa wiki.
Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma lililoanza kutumika hivi karibuni baada ya kukamilika kujengwa kwa fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit-JDU) Mhe. Zahra Maruma akiwatambulisha wajumbe aliombatana nao mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Mhe. Ilvin Mugeta (katikati).
Naibu Msajili wa Mahakama
Kuu Kanda ya Kigoma Mhe. Arnold Kirekiano akielezea kuhusu shughuli pamoja na wadau
mbalimbali wanaopatikana katika Jengo la Mahakama Kuu na mifumo iliyopo mbele
ya wajumbe wa Benki ya Dunia.
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Mawakili Mkoa wa Kigoma Bw. Ignatus Kagashe akielezea jambo.
Baadhi ya wajumbe
wakikagua matumizi ya vifaa (Public Address System) katika ukumbi wa wazi wa
Mahakama Kuu Kigoma
Picha ya pamoja ya wajumbe
wa benki ya Dunia pamoja na viongozi wa Mahakama Kanda Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni