Na
Catherine Francis – Mahakama, Arusha
Katibu
mkuu Wizara ya Sheria na Katiba, Prof. Sifuni Mchome amepongeza kasi ya
maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) unaoendelea
Jijini Arusha.
Pongezi
zimetolewa na Mchome alipotembelea na
kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, Julai 9, mwaka huu, ambapo alisema kulingana
na muda ambao limeanza kujengwa hadi sasa
hatua waliyofikia ni nzuri na inaridhisha.
‘‘Wahandisi
wanaohusika na ujenzi huu endeleeni na kasi hiyo na ikiwezekana mmalize mapema
zaidi kabla ya mwezi Desemba kama ilivyokubaliwa awali ili kuweza kuruhusu upatikanaji wa huduma za kisheria kwa haraka
na mapema zaidi,’’alisema Katibu Mkuu
huyo.
Aidha Mchome alipata nafasi ya kutembelea ofisi ya Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Mhe.
Moses Mzuna ili kuweza kujadili
mafanikio na changamoto za ujenzi huo.
Naye Mtendaji Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Bw.Edward Mbara, aliwasilisha ripoti ya ujenzi huo na kuzitaja changamoto kubwa walizokumbana nazo kuwa hali ya hewa ya mvua pamoja na ucheleweshaji
wa malipo kwa wakandarasi kutoka Hazina.
Akitatua
changamoto ya uchelewashaji wa malipo hayo, alipiga simu kwa wahusika papohapo
jambo ambalo lilipatiwa ufumbuzi na
kupewa majibu ya kuridhisha
Katika
ziara hiyo Mchome aliambatana na uongozi
wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Arusha
walitembelea ujenzi huo ili kujionea hali halisi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.
Sifuni Mchome( kushoto) akizungumza jambo kwenye ofisi za eneo la ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC)
unaoendelea Jijini Arusha, kushoto ni Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha Mhe. Moses Mzina.
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja. |
(Na Catherine Francis – Mahakama, Arusha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni