Na Rosena Suka, IJA-Lushoto
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Benhajj Shaaban Masoud amewataka
Wasaidizi wa Sheria wa Majaji kutumia vyema elimu ya
uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya
sheria na haki nchini.
Akifunga
rasmi Mafunzo hayo hivi karibuni yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto, Mhe. Jaji Dkt Masoud aliwaeleza washiriki kwamba, imani ya wananchi ni
kuwa, Mahakama ni mahali pa kupata haki, hivyo basi Maafisa wa Mahakama wanatakiwa
kutambua muhimu walionao kwa wananchi wanaowahudumia.
“Ninawasihi sana kujiepusha na rushwa, kataeni
rushwa, kemeeni rushwa na toeni elimu pale mnapopata nafasi na uwezo wa kufanya
hivyo juu ya madhara ya rushwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi”
Aidha,
aliendelea kwa kuwaomba Maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya
sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu anayopewa Jaji
husika kwa wakati na pia kwa viwango bora.
Kwa
upande mwingine, Mhe. Dkt Masoud aliwapongeza wawezeshaji wa mafunzo kwa jinsi
walivyoendesha mafunzo hayo kwa umahiri mkubwa.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt Benhajj Shaaban Masoud akifunga Mafunzo ya
namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa Wasaidizi wa Sheria wa
Majaji yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushotot, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
Jaji
wa Mahakama kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt Benhajj Masoud akimkabidhi Cheti
cha ushiriki Hakimu Mkazi Mhe. Edga Edom Mwaiswaga baada ya kumaliza mafunzo
hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni