Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Harold Nsekela enzi ya Uhai wake
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Harold Nsekela amefariki dunia leo asubuhi, Desemba 06, 2020 mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda Mfupi.
Taarifa
Zaidi kufuatia Msiba huo pamoja na taratibu nyingine za mazishi zitajulikana baadaye.
Marehemu
Jaji Mstaafu Nsekela alizaliwa Oktoba 21 mwaka 1944.
Wadhifa
wa Jaji
Marehemu Jaji Nsekela aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mwezi Februari mwaka 2003 marehemu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, nafasi aliyoitumikia mpaka alipostaafu kwa mujibu wa Sheria.
Marehemu
Jaji Harold Nsekela aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma mwezi Desemba, 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki
leo asubuhi.
Bwana
Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni