- · Ibada ya kuaga mwili yafanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay
- · Mwili wake wazikwa katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam
- · Jaji Maina atakumbukwa kwa Uadilifu, uchapakazi na uzalendo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Marehemu Jaji William Maina. Ibada ya kuaga mwili huo imefanyika leo Februari 24, 2021 katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jaji Mstaafu Maina.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Lameck mlacha akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Jaji Maina.
Baadhi ya ndugu wakiaga mwili wa mpendwa wao.
Sehemu ya ndugu wa marehemu wakiwa katika ibada ya kuaga mwili wa mpendwa wao.
Mapadri
wakiongoza ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu William Maina.
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma pamoja na baadhi ya Waheshimiwa
Majaji wakifuatilia ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jaji William Maina,
katikati ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi
na kushoto ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Lameck
Mlacha na wawili waliopo nyuma ni Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania.
Viongozi
na Maafisa mbalimbali wa Mahakama wakiwa katika ibada hiyo.
Mhe.
Jaji Mkuu akitoa risala yake mara baada ya ibada kukamilika, katika salaam zake
za rambirambi, Mhe. Jaji Mkuu amesema kuwa Marehemu Jaji Mstaafu Maina alikuwa
mchapakazi, muadilifu na mwenye kupenda ushirikiano katika kazi.
Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akitoa
salaam za rambirambi kwa familia, marehemu Jaji Maina aliwahi pia kufanya kazi
Sekretariat ya Maadili.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni