· Wasajili na Watendaji wa Mahakama watembelea mradi huo Dodoma
Na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma
Mradi wa ujenzi wa
jengo la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania unaojengwa katika eneo la ‘NCC Link’
jijini Dodoma unaendelea vizuri.
Akizungumza
na baadhi ya Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama waliotembelea mradi huo wa
ujenzi jana Aprili 14, 2021, Mhandisi Mkazi kutoka timu ya Washauri Elekezi,
Mhandisi Evarist Mushi alisema kuwa Mradi huu unajumuisha ujenzi wa majengo
matatu (3) yanayounganishwa na jengo la utawala.
Mhandisi
Mushi amesema kuwa mradi huu unajumuisha jengo la Mahakama ya juu ‘Supreme
court’ ambapo anaeleza kuwa jengo hili lipo katika hatua ya ‘floor’ ya chini ‘ground
floor’ ambapo nguzo zote zimekamilika pamoja na msingi wa jengo hilo.
“Kwa
upande wa jengo la Mahakama ya Rufani, lipo katika hatua ya ghorofa ya kwanza ‘first
floor’ ambao ‘elevated ground floor, ground floor, basement floor’ na msingi
tayari zimekamilika,” alisema Mhandisi Mushi.
Aidha,
kwa upande wa jengo la Mahakama Kuu, Mtaalamu huyo amesema kuwa msingi pamoja
na ‘floor’ za chini zimeshakamilika ambapo kwa sasa zinafungwa nguzo za kwenda
ghorofa ya kwanza ‘first floor’ ya jengo hilo.
Aliongeza
kuwa jengo la Makao Makuu ‘HQ’ lipo kwenye hatua ya msingi na maandalizi yote
ya chuma yapo tayari.
Kwa
mujibu wa Mtaalam huyo ujenzi wa mradi huu ulianza rasmi mwezi Julai, 2020 na
unatarajia kukamilika Desemba 2022.
Muonekano wa sehemu za jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania linaloendelea kujengwa jijini Dodoma.
Mhandisi
Mkazi kutoka timu ya Washauri Elekezi, Mhandisi Evarist Mushi (mwenye suruali
ya kaki) akizungumza na sehemu ya Naibu Wasajili, Watendaji wa Mahakama na
Maafisa wengineo wa Mahakama waliotembelea kujionea maendeleo ya Mradi wa ujenzi
wa Makao makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni