Jumatatu, 12 Julai 2021

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA KANDA YA DODOMA AFARIKI DUNIA

 TANZIA

Bi. Susana Fatina Joseph enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. Susana Fatina Joseph (59) (pichani) kilichotokea tarehe 10 Julai, 2021 katika Hospitali ya Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma.

Marehemu Susana alikuwa Msaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama ya Mwanzo Bereko iliyopo Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Bi. Maria Francis Itala inasema mazishi ya mtumishi huyo yalifanyika jana Julai 11, 2021 katika Kijiji cha Mondo kilichopo Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma.

Marehemu Susana aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tangu 01 Machi, 1982 akiwa Msaidizi wa Kumbukumbu cheo alichokitumikia kwa muda wake wote aliokuwa Mtumishi wa Mahakama katika vituo mbalimbali ikiwemo Mahakama ya Mwanzo Kondoa Mjini na Bereko na alitarajiwa kustaafu kazi kwa umri tarehe 07 Januari, 2022.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki wa mtumishi huyo katika kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni