Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 23 Agosti, 2022 ameshiriki katika zoezi maalum la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza nchini.
Mhe. Prof. Juma ameshiriki zoezi hilo kwa kuhesabiwa na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa alipomtembelea nyumbani kwake Oysterbay barabara ya Kajificheni jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa, “Kwa upande wa Mahakama, Sensa ni zoezi muhimu sana kwa sababu inatupa idadi sahihi ya watu itakayosaidia kuboresha zaidi huduma za utoaji haki kwa wananchi.”
Mhe. Prof. Juma alisema hivyo, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki katika zoezi hilo muhimu kwa uboreshaji wa huduma za utoaji haki na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
MATUKIO KATIKA PICHA JAJI MKUU WA TANZANIA, MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA ALIPOSHIRIKI ZOEZI LA SENSA.
Mahojiano yakiendelea kati ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye ni Mkuu wa Kaya na Karani wa Sensa, Bi. Yvonne Ngakongwa (kulia).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni