Jumatatu, 31 Oktoba 2022

JAJI MFAWIDHI MUSOMA AHIMIZA VIWANGO KATIKA MAJENGO YA MAHAKAMA

Na Francisca Swai, Mahakama-Musoma

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe.  Fahamu Mtulya amesisitiza wakandarasi wa majengo ya Mahakama ya Wilaya Rorya na Mahakama ya Mwanzo Kinesi kuzingatia viwango kwani ubora wa kazi zao ndio utakao watangaza hata katika miradi mingine ya baadae.

Mhe. Mtulya alitoa msisitizo huo katika siku ya nne ya ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za Mahakama wilayani Tarime na Rorya aliyoifanya hivi karibuni. Aliwahimiza wakandarasi hao kukamilisha miradi kwa wakati na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizoelekezwa kurekebishwa.

Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya Rorya kwa mbele.
Msimamizi wa mradi wa Mahakama ya Wilaya Rorya, Eng. Sydney Pius (mwenye kofia nyeupe) akieleza jambo kuhusiana na ukumbi wa wazi (Open Court).

Viongozi Kanda ya Musoma wakisikiliza maelezo ya msimamizi wa mradi, Eng. Sydney Pius kuhusiana na mfumo wa maji katika jengo la Mahakama ya Wilaya Rorya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe.  Fahamu Mtulya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine, akiwemo Naibu Msajili, Mhe. Frank Moshi (wa tatu kulia), Mtendaji wa Mahakama Bw. Festo Chonya (wa tatu kushoto), Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Tarime, Mhe. Yohana Myombo, (wa pili kulia), Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Shirati, Mhe. Boniphace Shimbe (wa kwanza kulia), Afisa Tawala Tarime, Bw, Herman Lomasi (wa pili kulia) na Msimamizi wa mradi kutoka Kampuni ya United Builders, Eng. Sydney Pius, (wa kwanza kulia).

Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Kinesi lilalojengwa na Mkandarasi PEK Brother ulioanza mwezi Januari 2022 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2022.
Viongozi wakifanya ukaguzi katika jengo la Mahakama ya Mwanzo Kinesi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni