Jumapili, 19 Novemba 2023

TIMU YA MAHAKAMA YA TANZANIA YAKAMILISHA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI LITHUANIA

Na. Tiganya Vincent-Vilnius- Lithuania

 

Ujumbe wa Mahakama ya Tanzania ukiongozwa na Mtendaji Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel tarehe 16 Novemba 2023 umekamilisha ziara ya mafunzo nchini Lithuania.

 

Ukiwa nchini humo ulijifunza uendeshaji wa masuala ya kiutawala wa Mahakama kutoka kwa Ofisi ya Kitaifa ya Uongozi wa Mahakama, Mpango Mkakati katika Mfumo  Mahakama Mtandao na Uhifadhi wa Taarifa za Kimahakama.

 

Maeneo mengine ambao ujumbe umebadilishana uzoefu katika kuimarisha usawa wa kijinsia mahakamani, uendeshaji wa mashauri kwa njia ya usuluhushi, uendeshaji wa huduma ya msaada wa kisheria na uboreshaji wa miundomibu ya Mahakama.

 

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo ya mafunzo ya siku nne, Prof. Ole Gabriel alisema katika mafunzo wamewasaidia kubadilishana uzoefu ambapo wamegundua kuwa yapo mambo mengine mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Mahakama wa Tanzania unawiana na ule wa Nchi ya Lithuania.

 

Alitaja baadhi mambo ambayo Mahakama ya Tanzania inawiano na ile Lithuani ni pamoja na kufunganisha mifumo ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano na wadau, mfumo wa Mahakama Mtandao ikiwemo uendeshaji wa mashauri kwa njia ya mtandao.

 

Ujumbe wa Mahakama Tanzania ulijumuisha Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo, Naibu Katibu Tume ya Utumishi wa Mahakama Alesia Mbuya na Mkurugenzi wa Kumbukumbu na Nyaraka Mahakama Kuu ya Tanzania, Malimo Thomas Manyambula.

 

Wengine ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri Desderey Kamugisha, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Allan Machela, Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Benjamin Mtesigwa na Naibu Msajili Mhe. Elimo Masawe.



 

Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmien(kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenefa Omolo wakati ziara ya mafunzo  kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika maeneo mbalimbali ya utoaji haki  kwa pande zote mbili.


 

Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmien(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenefa Omolo (kushoto) na Naibu Katibu Tume ya Utumishi wa Mahakama Alesia Mbuya wakati ziara ya mafunzo  kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika maeneo mbalimbali ya utoaji haki  kwa pande zote mbili.


 


Mtendaji wa Mahakama ya Tanzania Prof . Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza hivi karibuni na viongozi wa Kitaifa ya Uongozi wa Mahakama wa Nchi ya Lithuania wakati wa  ziara ya mafunzo katika ofisi hiyo.


 


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof . Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmien(kulia) wakati wa ziara ya mafunzo ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania nchini humo.

 


Rais wa Mahakama ya Wilaya ya Mji wa Vilnius nchini Lithuania, Mhe. Viktorija Šelmien (kushoto) akitoa maelezo kwa ujumbe wa Mahakama ya Tanzania hivi karibuni uliotembelea nchini hiyo kwa ajili ya kubadilisha uzoefu.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni