Jumatatu, 17 Juni 2024

JAJI MKEHA : TOENI TUZO ZINAZOTEKELEZEKA

 Na Naomi Kitonka-Mahakama

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara,Mhe.Cyprian Mkeha ametoa raia kwa mahakimu kutoa tuzo zinazotekelezeka ili kurahishisha utekelezaji wa hukumu na amri za mahakama.

 

Mhe.Mkeha alisema hayo tarehe 15 Juni, 2024 wakati akitoa mafunzo ya kubadilishana uzoefu kuhusu utekelezaji wa hukumu na amri za mahakama kwa mahakimu hao wa ngazi mbalimbali kwenye ukumbi wa mafunzo wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke,kilichopo jijini Dar es Salaam.

 

“Lengo la utekelezaji wa hukumu siyo kumdhalilisha mdaiwa, bali ni kumwezesha mshindi wa tuzo kupata haki yake anayostahili kuipata, aliyopewa na Mahakama.” alisema Jaji Mkeha.

 

Aliongeza kwamba mahakimu hao, wanapaswa kufanya utambuzi wa mali za mdaiwa ili kuweza kubaini uwezo wake kabla ya kutoa hukumu na amri za mahakama ili kuzifanya ziweze kutekelezeka.

 

“Ni lazima maombi mahususi yatumwe mahakamani ili mchakatowa utekelezaji wa hukumu ukamilike,ambapo maombi hayo yanawezwa kufanya na wakili,mshindi wa tuzo au mtu aliyehamishiwa tuzo, ambapo utambuzi wa mali ni muhimu ili kuweza kupunguza mganganyiko,” alisisitiza.

 

Awali akifungua mafunzo hayo Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC), Temeke Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kuwajengea uwezo mahakimu hao, kwa ubadilishana uzoefu.

 

Akifunga mafunzo hayo,Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. David Ngunyale alimpongeza Jaji Mkeha kwa mafunzo aliyoyatoa kwa kuwa yamesaidia kuwajengea uwezo mahakimu hao. Huku akiwataka mahakimu hao kwenda kutoa elimu waliyoipata kwa wengine.

 

“Uwezo mliojengewa ukaonekane kwenye hukumu zenu,’’ alisema Mhe. Jaji Ngunyale.

 

Mafunzo hayo yamewashirikisha Majaji wa Kituo hicho, Naibu Wasajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi na Mahakimu Wafawidhi.

 


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara,Mhe.Cyprian Mkeha akitoa  mada ya utekelezaji wa hukumu na amri za mahakama kwa mahakimu wa ngazi mbalimbali kwenye ukumbi wa mafunzo

wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke, jijini Dar es Salaam.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC), Temeke Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa(wa pili kulia) akifungua mafunzo ya utekelezaji wa hukumu na amri  za mahakama, (katikati) Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara,Mhe.Cyprian Mkeha,(wa kwanza kulia)ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania IJC Temeke,Mhe. Asina Omari, (wa pili kushoto) ni Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. David Ngunyale na (wa kwanza kushoto)ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania IJC Temeke,Mhe. Frank Moshi.

 


                                           Mahakimu wakiwa kwenye mafunzo.

 



Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania IJC Temeke,Mhe. Frank Moshi akitoa neno la utangulizi kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.

 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,Mhe.Aziza Hassan Mbadjo aliuliza swali kwenye mafunzo hayo.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Temeke,    Mhe. Ali Mkama akiuliza  swali kwenye mafunzo hayo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Watoto Kisutu,Mhe. Vicky Mwaikambo akiuliza swali.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. David Ngunyale(wa pili kushoto) akifunga mafunzo hayo.(Katikati) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara,Mhe.Cyprian Mkeha, Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (IJC), Temeke Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa(wa pili kulia),(wa kwanza kulia)ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania IJC Temeke,Mhe. Asina Omari na (wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, IJC Temeke,Mhe. Glady’s Nancy Barthy.

  Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na mahakimu.

 

(Picha na Magreth Kinabo-Mahakama)

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni