Ijumaa, 21 Juni 2024

MAHAKAMA YA TANZANIA TAYARI KUWAVAA BUNGE

  • Yaahidi kulichakaza Bunge

Na ARAPHA RUSHEKE NA JEREMIA LUBANGO - Mahakama, Dodoma

Timu ya Mahakama inayoundwa na Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu  imefanya mazoezi yake ya mwisho katika viwanja vya Shule ya St. Gasper Jijini Dodoma leo tarehe 21 Juni, 2024 kujiweka sawa na Bonanza la kimichezo lililoandaliwa na Bunge (Bunge Gland Bonanza).

Bonanza hilo litatimua vumbi kesho tarehe 22 Juni, 2024 katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.Mazoezi hayo yameongozwa  na Kocha Spear  Mbwembwe aliyekuwa Mchezaji wa Simba Sport Clubmwaka 1990-91.

Akizungumza katika viwanja hivyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma,Mhe. Fahamu Hamidu Mtulya, ambaye pia ni mmoja ya wachezaji wa timu hiyo, amewaomba Wadau na Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Bonanza hilo.

Mhe. Mtulya ametumia fursa hiyo kulipongeza Bunge kwa kuialika Mahakama katika Bonanza hilo, kwani kitu hicho hakikuwahi kutokea huko nyuma. Alisema kuwa Majaji wa Mahakama ya Tanzania nao ni Wanamichezo.

Kesho asubuhi kwenye Uwanja wa Jamuhuri hapa Dodoma mtajionea Majaji wakisaidiwa na Naibu Wasajili wanavyotandaza kabumbu la 3-5-2 wakiifunga timu ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mhe. Mtulya.

Naye Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mhe, John Kahyoza, ambae ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Manyara, amesema Bonanza hilo ambalo limejumuisha Mihimili mbalimbali, ikiwemo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni fursa ya pekee ya kufahamiana na kujenga umoja na kuamusha hamu ya kufanya mazoezi na maendeleo ya kujenga afya.

Alisema timu yake inashirikisha Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu na Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu. 

“Bonanza hili ni kubwa sana, liajumuisha Taasisi, Mihimili na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarlengolikiwa kushiriki mazoezi kwa maendeleo ya Taifa na ni  jambo jema na kubwa,” alisema Mhe.Kahyoza.

 

Timu ya Mahakama wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa na Bunge Gland Bonanza.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina akiwa katika mazoezi hayo.

Timu ya Mahakama wakiongozwa na Kocha Spear Dunia Bwembwe (aliyevaa kofia juu na chiniakikinoa kikosi chake.


Nahodha wa Timu  ya Mahakama (aliyevaa jaketi jeusi) akiwaongoza wachezaji wenzake katika mazoezi hayo.

Kikosi cha Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mazoezi asubuhi ya leo tarehe 21 Juni, 2024 katika viwanja vya Shule ya St. Gasper jijini Dodoma.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama. 




 

 

 

  

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni