Ijumaa, 11 Oktoba 2024

JAJI MFAWIDHI MBEYA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MAHAKAMA

Na DANIEL SICHULA - Mahakama Mbeya

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga amefanya ziara ya ukaguzi wa Mahakama za Wilaya ya Chunya na Mbalali ikiwemo Mahakama za Mwanzo Chunya, Rujewa, Chimala, Igurusi na Ilongo na kupokea taarifa za utendaji kazi vilevile na kufanya vikao na watumishi wa Mahakama wa vituo hivyo vya kazi.

Katika ziara hizo zilizofanyika hivi karibuni mwezi Oktoba, 2024 Mhe. Tiganga alipata wasaa wa kupokea taarifa za utendaji kazi wa Mahakama hizo za Wilaya pamoja na Mahakama za Mwanzo, zilizofafanua baadhi ya mafanikio na changamoto katika utendaji kazi matahalani uchakavu wa majengo ya Mahakama, upungufu wa watumishi na sehemu ya mejengo ya kutolea huduma kukosa umeme.

Mhe. Tiganga aliwapongeza watumishi wa Mahakama za Wilaya hizo kwa jitihada wanazofanya katika kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani na pia mpango mkakati waliojiwekea wa kupunguza mahabusu gerezani na kupelekea idadi ya mahabusu kupungua kwenye magereza mkoa wa Mbeya.

“Kabla hatujachukua hatua za kushirikiana na wadau wa Mahakama kujenga gereza hapa wilayani Chunya ni muhimu kuanza kwa kupunguza mahabusu gerezani hasa Gereza la Ruanda Mbeya ambalo lina idadi kubwa ya mahabusu na wafungwa waliopo ukilinganisha na uwezo wake” alisema Mhe. Tiganga.

Vilevile, Mhe. Tiganga aliwasisitiza Mahakimu Wafawidhi kushughulikia mashauri ya mirathi kwa weledi na uadilifu na pia kuhakikisha wanufaika wa mirathi hiyo wanalipwa stahiki zao kwa wakati na kuwahimiza wanufaika hao kufunga mashauri hayo baada ya kukamilika kwa taratibu husika.

“Moja ya vipaumbele vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya ni kuhakikisha wanufaika wa mirathi wanalipwa, na kwamba wasipolipwa kwa wakati inaleta taswira kwamba Mahakama ina miliki fedha nyingi ambazo hazina maelezo na kupelekea Mahakama kupata hati chafu kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu,” aliongeza Jaji Mfawidhi.

Akizungumza katika vikao alivyofanya na watumishi wa Mahakama hizo, Mhe. Tiganga aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi kawa bidii, ushirikiano na upendo hasa wakiongozwa na salamu ya Mahakama ambayo ni nguzo ya utendaji kazi mahakamani ya “Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji” ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi katika utoaji haki.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Chunya Mhe. James Mhanusi, aliipongeza Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya kwa msaada mkubwa walioupata wa kukabidhiwa chombo cha usafiri pamoja na kuongezewa mtumishi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (kulia) akikagua rejista za mashauri wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mahakama. Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (mbele) akiwa ameshika kitabu cha wageni wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga akiwa akisaini kitabu cha wageni wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (kushoto) akisalimiana na watumishi  wa Mahakama wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (aliyenyoosha mikono) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo. 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mahakama wakati wa ziara hiyo.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mahakama wakati wa ziara hiyo.

Sehemu ya watumishi wa Mahakama wakimsikiliza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (hayupo pichani) wakati wa ziara hiyo.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtumishi (hayupo pichani) wakati wa ziara hiyo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (kushoto) akiwa kwenye viwanja vya Mahakama wakati wa ukaguzi huo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga (kushoto) akisalimiana na watumishi  wa Mahakama wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa Mahakama.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni