Na Daniel Sichula – Mahakama, Mbeya
Klabu
ya mazoezi ya watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya mnamo tarehe
9 Novemba, 2024 walishiriki katika tamasha la bonanza lililofanyika kwenye
viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA) jijini Mbeya na kujinyalia medali mbalimbali
na kutangazwa kuwa washindi wa jumla katika bonaza hilo.
Bonaza
hilo lililoandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya
lilialika vikundi mbalimbali vya michezo jijini Mbeya ikiwemo Klabu ya mazoezi
ya Mahakama Kuu Kanda Mbeya kushiriki katika tamasha hilo la michezo.
Watumishi
hao waliongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya ambaye pia ni
mlezi wa klabu ya michezo ya Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles
Tiganga katika kushiriki michezo mbalimbali iliyokuwa imeandaliwa katika bonaza
hilo.
Aidha,
miongoni mwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya walioungana na watumishi
klabu hiyo alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Aisha
Sinda aliyekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watumishi wanashiriki na kujizolea
medali nyingi zilizoandaliwa katika bonaza hilo.
Michezo
iliyowapa ushindi wa jumla Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ilikuwa kuvuta kamba kwa
upande wa wanaume na wanawake na ikiibuka kidedea kwenye michezo yote miwili.
Ushindi
huo wa michezo mbalimbali ulitoa hamasa kwa watumishi wa Mahakama kujiunga
kwenye klabu ya mazoezi, kwani mazoezi yamekua chachu ya kuwaleta watumishi
pamoja na kujenga afya ya mwili na akili.
Wakati
huo huo, Mwenyekiti wa klabu ya mazoezi Mahakama Kuu Mbeya Bw. Emmanuel
Mwalyagile alitoa ratiba ya mazoezi kwa watumishi wapya waliojiunga na klabu ya
mazoezi kuwa ni siku ya Jumanne na Ijumaa kwa wiki.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni