Na. SALUM TAWANI –Mahakama, Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel leo tarehe 4 Novemba, 2024 amefika msibani nyumbani kwa Marehemu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mussa Kipenka Madale jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa salamu za pole.
Marehemu Kipenka alifikwa na umauti tarehe 2 Novemba, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Prof. Ole Gabriel amewapa pole wanafamilia na kusema kuwa Mahakama ya Tanzania imepoteza mtu makini ambaye alikuwa bado ana mchango mkubwa kwa Mhimili huo na Taifa kwa ujumla kwa kuwa bado walikuwa wanaendelea kupata maarifa kutoka kwake ijapokuwa alikuwa ameshastaafu katika utumishi wa umma.
‘’Marehemu Jaji Mstaafu na wengineo ambao wamestaafu katika utumishi wa umma bado huwa tunapata maarifa kutoka kwao katika kuendesha Muhimili huu wa Taifa, hivyo tumepoteza nguzo muhimu sana katika kuendeleza utendaji kazi katika Mhimili na Taifa kwa ujumla,” amesema.
Mtendaji Mkuu alifanikiwa pia kukutana na Mama wa Marehemu, Bi. Anna Thomas Mussa na kumsihi, “hii ni njia yetu sisi sote, hivyo hatuna budi kumuombea marehemu Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.”
Naye mdogo wa Marehemu, Bi.Ukende Mwigo Mussa alimshukuru Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kuwa na moyo wa upendo na kwenda kuwapa pole na kuwafariji. “Mmetutia moyo kwa kweli katika kipindi hiki kigumu tulicho nacho kwa sasa, Mungu azidi kuwabariki na kuwa na moyo huu wa upendo,” alisema.
Mwili wa Marehemu utaagwa kesho katika Kanisa la K.K.T Wazo Hili saa nane mchana na baada ya hapo utasafirishwa kwenda kijijni kwao Kinampanda mkaoni Singida kwa ajili ya mazishi siku ya tarehe 6 Novemba, 2024.
Katika picha wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasili nyumbani kwa Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Mussa Kipenka na wa kwaza kulia ni Afisa Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Peter Machalo.
Katika picha wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akimfariji mdogo wa marehemu, Bi. Ukende Mwigo Mussa.
Katika picha wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel na katikati ni Mama wa Marehemu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mussa Kipenka na wanandugu.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa na mdogo wa Marehemu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mussa Kipenka alipowatembelea kuwapa pole kutokana na msiba huo.
Katika picha wa kwanza kushoto ni Mke wa Marehemu, Bi. Rehema Kipenka Mussa akipokea salam za pole kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel.
Katika picha wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwapa pole wafiwa nyumbani kwa Marehemu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mussa Kipenka.
Baadhi ya ndugu wakijadiliana jambo katika msiba wa Marehemu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mussa Kipenka.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni