TANZIA
Marehemu Kambona Halifa Kamwenye enzi za uhai wake.
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mlingoti ilioko katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Bw. Kambona Halifa Kamwenye aliyekuwa akihudumu katika Mahakama hiyo kwa Cheo cha Mlinzi Mkuu.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Songea, Bw. Allan Mwella marehemu Kambona alifikwa na umauti jana tarehe 30 Desemba, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Bw. Mwella amesema kuwa, kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ameongeza kwamba, msiba upo nyumbani kwa marehemu, Kijiji cha Sisi kwa Sisi kilichopo katika Wilaya ya Tunduru huku taratibu za mazishi zikiendelea kuratibiwa kwa kushirikiana na familia.
Mtendaji huyo amebainisha kuwa, maziko yanatarajiwa kufanyika leo Jumanne tarehe 31 Desemba, 2024 nyumbani kwa marehemu.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni