Na Fredrick Mahava - Mahakama, Sumbawanga.
Makabidhiano
ya mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo iliyopo mkoani Rukwa yalifanyika
hivi karibuni kati ya Viongozi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga, Mkandarasi
Mshauri MD Consultants JV Mhandisi na Mkandarasi wa Ujenzi Works Contractors
Ltd.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya mradi huo kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Mahakama hiyo
ya Wilaya ya Kalambo ambaye ni Kampuni ya Works Contractors Ltd. Mtendaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Elias Essaba alimtaka Mkandarasi
huyo kuzingatia masharti ya Mkataba ikiwa ni pamoja na kumaliza mradi huo wa
ujenzi ndani ya muda uliyoainisha kimkataba.
Naye,
Mshauri wa ujenzi wa mradi huo kutoka kampuni ya MD Consultants JV Mhandisi
alifafanua kuwa, vipengele vyote vya Mkataba wa ujenzi huo vitazingatiwa
ipasavyo kwa ushauri na usimamizi wa karibu ili kuhakikisha kwamba Mkandarasi
kutoka kampuni ya Works Contractors Ltd anamaliza kazi hiyo ya ujenzi kwa
wakati uliopangwa kwenye mkataba.
Kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kalambo ujezi huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi nane ambayo ni sawa na siku 240 za kimkataba wakati ambao mkandarasi anapaswa kukabidhi jengo hilo kwa mteja ambaye ni Mahakama ya Tanzania.
Aidha,
wakati wa makabidhiano hayo Mtendaji Bw. Essaba aliambatana na Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Wilaya Kalambo Mhe. Nickson Temu, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya
Mwanzo Matai Mhe. Suzan Mkinga, Mhandisi wa Mahakama kutoka Makao Makuu ya
Mahakama na Afisa Utumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo Bw. Samwel Kamese.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Elias Essaba (aliyevalia tai) akikabidhi nyaraka muhimu za ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kalambo ikiwemo michoro na mkataba wa ujenzi wa jengo hili kwa Mkandarasi wa Ujenzi kampuni ya Works Contractors Ltd.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni