Na DOTTO NKAJA-Mahakama, Geita
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Kevin Mhina hivi karibuni alifanya ziara katika
Gereza la Geita ili kusikiliza changamoto kutoka kwa Wafungwa na Mahabusu.
Akiwa katika Gereza hilo,
Mhe. Mhina alisikiliza changamoto mbalimbali ikiwemo Wafungwa kucheleweshewa
nakara za hukumu, vitabu kutotolewa kwa wakati na mfumo wa kusajili mashauri
kwa njia ya mtandao kuwa changamoto kwa Wafungwa na Mahabusu.
Changamoto nyingine ni upande
wa Jamhuri kuchelewesha kuleta mashahidi kwa wakati na kesi zinazoshushwa
kutoka Mahakama ya Rufani kurudishwa Mahakama Kuu kutopangiwa muda wa
kusikilizwa kwa wakati.
Akitroa ufafanuzi wa
changamoto hizo, Mhe. Mhina alisema changamoto ya mifumo kwa sasa siyo kisingizio
cha kuchelewesha kutoa uamuzi katika utoaji haki, bali ni watumiaji wenyewe
ndiyo wanaochelewesha kwa kushindwa kufuata utaratibu.
Aidha, aliwahimiza upande
wa Jamhuri kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuhakikisha haki inatolewa
kwa wakati, hivyo kuondokana na changamoto hizo.
Katika ziara hiyo, Jaji Mfawidhi aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Fredirick Lukuna, Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Geita, Bi. Masalu Kisasila, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Mhe. Cleofas Wanne, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Geita, Mhe. Salius Muchunguzi na Maofisa kutoka Vyombo vya Dora.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Kevin Mhina akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Geita.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Geita, Mhe. Kevin Mhina-juu na chini- akisikiliza na kutoa ufafanuzi wa changamoto kwa Wafungwa na Mahabusu Wanawake na Wanaume-hawapo kwenye picha- katika Gereza la Wilaya ya Geita.
Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa
wa Geita, Afande Lusajo Mwasalyanda akitoa ufafanuzi wa mambo fulani wakati wa ziara
hiyo.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni