Jumanne, 3 Februari 2026

MAHAKAMA NA WADAU WA HAKI WASHIRIKI KILELE CHA SIKU YA SHERIA SONGWE

Na. IMAN MZUMBWE – Mahakama, Songwe

Siku ya Sharia nchini ni jukwaa muhimu la kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama na Taasisi za haki pamoja na kukuza utawala bora na haki nchini, kuimarisha uelewa kwa wananchi kuhusu haki, wajibu na misingi ya utawala bora wa kisheria nchini.

Maadhisho hayo yamefanyika Jana tarehe 2, Feburuari 2026 katika ukumbi wa Mpende Jilani uliopo Wilaya Mbozi Mkoani Songwe, Maadhimisho hayo yamefanyika pia katika Mahakama za Wilaya Momba, Ileje na Wilaya Songwe.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe Mhe. Nemes Chami alisema kuwa, dhamira ya Mahakama ni kuendelea kutoa huduma bora za haki kwa wanachi wote.

Aidha, Mhe. Chami aliongeza kwa kusema kuwa mifumo ya TEHAMA mahakamani imesaidia kurahisisha utendaji kazi na kuongeza kasi juu ya usikilizwaji wa mashauri na kupunguza ya mlundikano wa mashauri mahakamani.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mhe. Moses Mwampashi alisisitiza umuhimu wa wananchi kufahamu haki zao za kikatiba na kutumia njia za kisheria katika kutatua migogoro, alihimiza wananchi kufuata ushauri wa kisheria mapema ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Makame alipongeza mapinduzi ya Mahakama katika mifumo ya TEHAMA na kusema Serikali imeweka nguvu kubwa na kipaumbele katika kuhakikisha Mahakama inafikia malengo yake na mifumo ya utendaji kazi.

Vilevile, Mhe. Makame aliwapongeza Viongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kuimarisha mifumo mizuri ya utoaji haki na kuimarisha utendaji kazi wa Mahakama. Aidha aliongeza kuwa, Mawakili wa Kujitegemea na Mawakili wa Serikali wana jukumu la kuisaida Mahakama katika zoezi la utoaji haki kwa wananchi.

Maadhimisho hayo yalihudhuliwa na wadau mbalimbali wa haki kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Huduma kwa jamii, Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Songwe (NPS) pamoja na Taasisi zingine za umma.

Kaimu Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Makazi Songwe Mhe. Nemes Chami akizungumza juu ya dhamira ya mahakama katika kuendelea kutoa huduma bora na za haki kwa wananchi wote.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Makame akizungumza na kupongeza Mahakama juu ya mapinduzi ya matumizi ya TEHAMA na mifumo ya utoaji haki kwa wakati kwa wananchi.

Mwakilishi wa Chama Cha Mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS) Mhe. Moses Mwampshi akizungumza na kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutumia njia za kisheria katika kutatua migogoro yao.

Kaimu Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Makazi Songwe Mhe. Nemes Chami (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa Songwe Mhe.Jabiri Makame (wa tatu kulia)  Wakili wa kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyiaka (TLS) (wa kwanza kulia) Mhe.Moses Mwampashi na Chief Nzunda wa kwanza kutoka (kushoto).

Sehemu ya picha ya pamoja ya wadau wa utoaji haki Mkoa Songwe waliokuwa wamehudhuria katika maadhisho ya siku ya sharia nchini.

Sehemu ya watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe  na Mahakama ya Wilaya Mbozi wakifatilia hotuba zinazotolewa katika maadhimisho hayo.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha -Mahakama)




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni