Na. IMAN MZUMBWE – Mahakama, Songwe
Siku
ya Sharia nchini ni jukwaa muhimu la kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama
na Taasisi za haki pamoja na kukuza utawala bora na haki nchini, kuimarisha uelewa
kwa wananchi kuhusu haki, wajibu na misingi ya utawala bora wa kisheria nchini.
Maadhisho
hayo yamefanyika Jana tarehe 2, Feburuari 2026 katika ukumbi wa Mpende Jilani
uliopo Wilaya Mbozi Mkoani Songwe, Maadhimisho hayo yamefanyika pia katika
Mahakama za Wilaya Momba, Ileje na Wilaya Songwe.
Akizungumza
katika Maadhimisho hayo Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe
Mhe. Nemes Chami alisema kuwa, dhamira ya Mahakama ni kuendelea kutoa huduma
bora za haki kwa wanachi wote.
Aidha,
Mhe. Chami aliongeza kwa kusema kuwa mifumo ya TEHAMA mahakamani imesaidia kurahisisha
utendaji kazi na kuongeza kasi juu ya usikilizwaji wa mashauri na kupunguza ya mlundikano
wa mashauri mahakamani.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mhe. Moses
Mwampashi alisisitiza umuhimu wa wananchi kufahamu haki zao za kikatiba na
kutumia njia za kisheria katika kutatua migogoro, alihimiza wananchi kufuata
ushauri wa kisheria mapema ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Makame alipongeza mapinduzi ya Mahakama
katika mifumo ya TEHAMA na kusema Serikali imeweka nguvu kubwa na kipaumbele
katika kuhakikisha Mahakama inafikia malengo yake na mifumo ya utendaji kazi.
Vilevile,
Mhe. Makame aliwapongeza Viongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kuimarisha mifumo
mizuri ya utoaji haki na kuimarisha utendaji kazi wa Mahakama. Aidha aliongeza
kuwa, Mawakili wa Kujitegemea na Mawakili wa Serikali wana jukumu la kuisaida Mahakama
katika zoezi la utoaji haki kwa wananchi.
Maadhimisho
hayo yalihudhuliwa na wadau mbalimbali wa haki kutoka Chama cha Wanasheria
Tanganyika (TLS), Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya
Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Huduma kwa jamii, Ustawi wa Jamii na Ofisi ya
Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Songwe (NPS) pamoja na Taasisi zingine za umma.
Kaimu
Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Makazi Songwe Mhe. Nemes Chami akizungumza juu
ya dhamira ya mahakama katika kuendelea kutoa huduma bora na za haki kwa
wananchi wote.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Makame akizungumza na kupongeza Mahakama juu ya
mapinduzi ya matumizi ya TEHAMA na mifumo ya utoaji haki kwa wakati kwa
wananchi.
Mwakilishi
wa Chama Cha Mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS) Mhe. Moses Mwampshi
akizungumza na kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutumia njia za kisheria
katika kutatua migogoro yao.
Kaimu Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Makazi Songwe Mhe. Nemes Chami (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa Songwe Mhe.Jabiri Makame (wa tatu kulia) Wakili wa kujitegemea kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyiaka (TLS) (wa kwanza kulia) Mhe.Moses Mwampashi na Chief Nzunda wa kwanza kutoka (kushoto).
Sehemu
ya picha ya pamoja ya wadau wa utoaji haki Mkoa Songwe waliokuwa wamehudhuria
katika maadhisho ya siku ya sharia nchini.
Sehemu
ya watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe
na Mahakama ya Wilaya Mbozi wakifatilia hotuba zinazotolewa katika
maadhimisho hayo.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni