MAHAKAMA YA TANZANIA YANG’ARA KIMATAIFA KATIKA UTAALAMU WA MATUMIZI YA AKILI UNDE
- Wasilisho la Jaji Dkt. Adam Mambi lawavutia wengi
Na Mwandishi-Mahakama
Mahakama
ya Tanzania imeng’ara Kimataifa katika utaalamu wa matumizi ya Akili unde
(Artificial Inteligence) na ushahidi wa teknoljia unaotokana na Akili unde
baada ya Wasilisho lililofanywa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Kanda ya Tabora Mhe. Dkt. Adam Mambi kuvutia wengi.
Jaji
Mambi aliwasilisha Mada kuhusu matumizi ya akili unde na namna kupokea na
kuchambua Ushahidi wa kielektroniki unaozalishwa na akili unde mahakamani
wakati wa Mafunzo ya Matumizi ya Akili unde kwenye utoaji wa haki
mahakamani yaliyofanyika hivi karibuni
jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Aidha,
Jaji Mambi ambaye pia ni Mtaalam wa Sheria za Tehama, Usalama Mtandaoni na
Akili unde alialikwa kutoa mada kwenye Mafunzo ya Matumizi ya Akili Unde katika
utoaji wa haki mahakamani ya Majaji, Mahakimu na Wanasheria wa Zimbabwe ambayo pia
yaliwahusisha wanasheria wa nchi za Afrika kusini, Ethiopia na Kazakhstan.
.
Akitoa Mada hiyo kwa Majaji na Mahakimu
zaidi ya 120 katika Mafunzo hayo, Jaji Mambi aliwafundisha aina mbalimbali za
ushahidi unaotokana na matumizi ya akiliunde na changamoto watakazokutana nazo
katika kupokea na kuchambua ushahidi unaotengenezwa au unaoboreshwa kwa kutumia
akiliunde.
Akitoa
mifano ya kesi kutoka nchi Mbali Mbali, Mheshimiwa Dkt. Mambi pia aliwaeleza juu ya masharti na misingi ya kisheria
inayohusu upokeaji na uchambuzi wa ushahidi wa kielektroniki akilinganisha na ushahidi
unaozalishwa na akiliunde kama vile sauti, picha, video, Ushahidi uliotengenzwa
kwa kutumia akili unde pamoja na changamoto zake.
Katika
mada hiyo, Jaji Mambi pia alielezea juu ya nafasi ya Akiliunde katika
kusuluhisha migogoro nje ya Mahakama (ADR) na katika tasnia ya Miliki bunifu
(Intellectual Property). Aidha, Washiriki hao pia walijifunza aina mabalimbali
za Ushahidi wa kielektroniki unaotokana na Akiliunde na namna ya kubaini
taarifa za kutungwa au ushahidi wa kutengenezwa kwa kutumia teknolojia feki (Deepfake).
Jaji
Mfawidhi huyo pia walifundisha namna ya kutumia Akiliunde kubaini kesi za
uwongo zinazoweza kuwasilishwa na mawakili wanaotumia akiliunde pasipo
kujiridhisha huku akitoa mifano ya kesi mbalimbali toka nchi mbalimbali
duniani.
Katika
mafunzo hayo, Mhe. Dkt. Mambi pia aliwafundisha washiriki juu ya nafasi ya
Mahakama katika kutafsiri Sheria na sera zinazogusa akili unde pamoja na kuweka
misingi endelevu wakati wa kutoa maamuzi yao. Aidha, washiriki walijifunza kwa
vitendo namna ya kutumia zana za akiliunde (AI Tools) katika kufanya utafiti,
Kuchambua kesi na kuandaa maamuzi.
Mada
nyingine zilizowasilishwa kwenye mafunzo hayo ni pamoja na Maadaili ya Taaluma
(Professional Ethics) katika matumizi ya akili unde, taarifa za faragaha (Data
Protection), Usalama mtandaoni (Cyber Security) na Miliki bunifu (Intellectual
Property) katika tasnia ya Akili
Unde.
Akifunga mafunzo hayo, Jaji Mkuu wa Zimbabwe
Mhe. Luke Malaba alimshukuru Jaji Mambiambaye ni mbobezi wa kimataifa katika
masuala ya akiliunde na TEHAMA kwa mafunzo mazuri aliyotoa yatakayowasaidia
Majaji na Mahakimu wa Zimbabwe katika kurahisisha kazi zao za utoaji wa haki.
Aidha Malaba pia alimshukuru Jaji Mkuu wa
Tanzania kwa kumruhusu Jaji Mambi Kwenda kutoa mafunzo Zimbabwe na kuahidi kuimarisha
ushirikiano zaidi na Mahakama ya Tanzania. Alisema kuwa Majaji wanahitaji
mafunzo kwa vitendo katika maeneo ya tekonolijia zinazoibuka kwa kasi kama
akili unde.
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo
waliishukukuru Mahakama ya Zimbabwe kwa kualika mtaalamu Sheria za Mitandao na
Akiliunde aliyetoa mafunzo ya aina yake kwa vitendo zaidi.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Matumizi ya Akili Unde katika utoaji wa haki mahakamani wakiwa kwenye Mafunzo hayo mjini Victoria Falls nchini Zimbabwe.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni