Na. MWINGA MPOLI – Mahakama, Mbeya
Katika
kuadhimisha Wiki ya Usuluhishi nchini Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya
imeungana na Kanda zingine nchini kuadhimisha wiki ya Usuluhishi kuanzia tarehe
13 Aprili, 2026 hadi tarehe 17 Aprili, 2026 yenye kaulimbiu isemayo, “Kutumia
Njia Mbadala ya Utatuzi wa Migogoro kama Mbinu Inayopendelewa ya Kutatua
Migogoro nchini Tanzania”.
Katika
maadhimisho hayo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim
Charles Tiganga, Naibu Wasajili pamoja na Mahakimu wameweka mkakati wa kupokea
na kusajili migogoro mbalimbali ihusuyo ardhi, ndoa na madai ya kawaida na
kuwapangia wasuluhishi wenye nyenzo za usuluhishi kwa ajili ya kuitatua
migogoro hiyo.
Mbali
na hilo Uongozi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya umeweka dawati maalumu la
kupokea migogoro katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya pamoja na
kuandaa vyumba maalumu vitakavyotumika kufanya usuluhishi.
Wananchi wote waliokuwa wamejitokeza walianza
kwa kupatiwa elimu ya usuluhishi na misingi yake, ambapo wananchi walipata
nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa kina juu ya masuala mbalimbali
ya kisheria yanayohusu usuluhishi wa migogoro.
Sehemu
ya watumishi na Mawakili wa Serikali wanaoshiriki katika maadhimisho hayo
Sehemu ya watumishi na Mawakili wa Serikali wanaoshiriki katika maadhimisho hayo
Wananchi
waliofika mahakamani wakipatiwa elimu ya usuluhishi inayoadhimishwa Kanda ya
Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni