Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya
Aliyekuwa
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim
Tiganga, tarehe 17 Juni, 2026 alimkabidhi rasmi Ofisi Jaji Mfawidhi mpya wa
Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya baada ya kuripoti katika
kituo chake hicho kipya cha kazi.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano, Mhe. Tiganga alitoa shukrani zake za dhati kwa
viongozi na watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya na kumpongeza Mhe.
Mtulya kwa kukabidhiwa majukumu hayo na kumtakia heri na mafanikio katika
utekelezaji wa majukumu ya kuiongoza Masjala hiyo ya Mbeya.
Hafla
hiyo ya makabidhiano ya Ofisi ilifanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya, ikihudhuriwa na aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga, Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya
Mbeya Mhe. Mussa Pomo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi.
Mavis Miti na Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya Mkoa wa Mbeya.
Makabidhiano
hayo yalijikita katika kukabidhi majukumu ya kiutawala, nyaraka mbalimbali za
ofisi, na taarifa muhimu za utendaji kazi, zote zikiwa na lengo la kuhakikisha
mwendelezo wa utoaji wa huduma za kimahakama na usimamizi wa shughuli za
Mahakama katika Masjala Ndogo ya Mbeya.
Kwa
upande wake, Mhe. Mtulya aliahidi kuendesha ofisi hiyo kwa weledi, kuendeleza
ushirikiano baina ya watumishi na kuimarisha upatikanaji wa huduma za haki kwa
wananchi wanaotumia Masjala hiyo ya Mbeya.
Makabidhiano
hayo yanaashiria mwanzo wa awamu mpya ya uongozi katika Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya, huku yakisisitiza dhamira ya kuendeleza ufanisi, uwazi na ubora
katika utoaji wa huduma za Mahakama kwa wananchi.
Jaji Mfawidhi mpya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, (kushoto) na aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (kulia) wakikabidhiana Ofisi katika kituo cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.
Jaji Mfawidhi mpya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya
Mhe. Fahamu Mtulya, (kushoto) na aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya Ofisi na kulia ni Jaji waMahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo akishuhudia kitendo hicho.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (kulia) akimpa kipande cha keki Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (kushoto) ikiwa ni ishara ya kumkaribisha.
Sehemu ya watumishi walioshiriki katika katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Ofisi
Sehemu ya watumishi walioshiriki katika katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Ofisi
Aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya
Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akikabidhiwa zawadi na Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (kushoto).
Aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya
Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akikata keki ya kuagwa katika hafla hiyo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akikata keki ya ukaribisho katika hafla hiyo.
Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya
Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akipokelewa na Viongozi na watumishi wa Mahakama Kuu Masjala
Ndogo ya Mbeya.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni