Na ELEOTHERIUS PONERA -Mahakama, Iringa
Mahakama ya Rufani ya
Tanzania iliyokuwa inaketi katika Masjala Ndogo ya Iringa, imekamilisha jukumu
lake kwa ufanisi baada ya kushughulikia jumla ya mashauri 59 kwenye kikao
kilichoanza tarehe 5 Oktoba, 2026 na kumalizika tarehe 30 Octoba, 2026.
Mahakama hiyo ilikuwa na
Majaji wanne, wakingozwa na Mhe. Jacobs Mwambegele, aliyekuwa Mwenyekiti wa
Jopo. Majaji wengine waliokuwepo ni Mhe. Dkt Paul Kihwelo, Mhe. Leila Mgonya na
Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim.
Akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa kikao hicho, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe.
Dianes Lymo, alisema kuwa jumla ya mashauri 59 yalipangwa kusikilizwa, ikiwemo
rufaa za jinai 24 , rufaa za madai 12, ombi moja la jinai na maombi ya madai 22.
“Kati ya hayo, mashauri
30 yalikuwa ni kesi za mzigo wa nyuma (Backlog) na 29 ni kesi za kuzuia mzigo
(Back-stopping). Katika mwenendo wa usikilizaji, mashauri yote 59 yaliyopangwa,
yalisikilizwa yote kwa asilimia 100,” alisema.
Mhe. Lyimo alieleza zaidi
kuwa kati ya hayo, mashauri 44 yameamuliwa, mashauri nane yanasubiri maamuzi na
mashauri saba yameahirishwa kwa sababu mbalimbali.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni