Jumanne, 3 Novemba 2026

MSAJILI MKUU MAHAKAMA AFANYA ZIARA MAHAKAMA YA MWANZO LUGOBA, MSATA

 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya amefanya ziara ya kikazi katika Mahakama ya Mwanzo Lugoba/Msoga na Mahakama ya Mwanzo Msata zilizopo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Katika ziara hiyo ya kikazi aliyofanya tarehe 02 Novemba, 2026, Mhe. Nkya ameweza kujionea namna Mahakama ya Mwanzo Lugoba/Msoga ilivyotetekea kwa moto usiku wa tarehe 06 Aprili, 2026 na kujionea uharibifu uliotokea.

Baada ya kuona uharibifu huo alipata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Mahakama hiyo na pia kuelekea katika Mahakama ya Mwanzo Msata amabapo shughuli za Mahakama ya Wilaya Bagamoyo iliyokuwa ikikaa katika Mahakama hiyo kuhamishiwa Mahakama ya Mwanzo Msata.


Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (wa kwanza kushoto) akikagua jengo la Mahakama ya Mwanzo Lugoba/Msoga iliyoteketea kwa moto  mnamo mwezi Aprili, 2026 (anayefuata) Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Livin Lyakinana na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani Mhe. Emmael Lukumai.


Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (katikati) baada ya kutembelea jengo la Mahakama ya Mwanzo Msata ambapo Huduma za Mahakama ya Wilaya Bagamoyo zilizokuwa zinapatika katika jengo la Mahakama ya Mwanzo Lugoba/ Msoga baada ya kuteketea kwa moto. Wa pili kushoto ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Livin Lyakinana na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Mhe. Emmael Lukumai (wa kwanza kushoto), Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es salaam Bi. Neema Mwasyoge na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo na watumishi wa Mahakama ya Msata, Wilaya na Mkoa wa Pwani.

Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (wa kwanza kushoto) akiangalia ukumbi wa Mahakama ya wazi ya Mahakama ya Mwanzo Msata, wa pili kulia ni Naibu Msajili Mfawidhi Mhe. Livini Lyakinana, wa pili kushoto ni Naibu Msajili na Katibu wa Msajili Mkuu, Mhe. Dkt. Jovin Bishanga (anayefuata) Mhe. Jovin na wa kwanza kulia ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Mhe. Emmael Lukumai. 

Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Lugoba/Msoga wakimsikiliza Msajili Mkuu (hayupo katika picha).

Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya (Kushoto) akiendelea kufanya ukaguzi katika eneo la Mahakama iliyoteketea kwa moto. Katikati ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Livin Lyakinana na kulia ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Mhe. Emmael Lukumai.

 Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya akisaini kitabu cha wageni  katika Mahakama ya Mwanzo Lugoba/ Msoga alipowasili kwa ziara ya kikazi.

Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Mahakama ya Mwanzo Msata kwa ziara ya kikazi. 

Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya na wajumbe alioambatana nao walipowasili Mahakama ya Mwanzo Lugoba/ Msoga tarehe 02 Novemba, 2026.

(Picha na EUNICE LUGIANA, Mahakama-Kibaha)





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni