Jumatatu, 9 Novemba 2026

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA, BW. EDMUND GABRIEL DYAMWALE AFARIKI DUNIA

TANZIA


MTUSHISHI BW. EDMUND GABRIEL DYAMWALE ENZI ZA UHAI WAKE.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mwanza inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Bw. Edmund Gabriel Dyamwale ambaye alikuwa akihudumu kama Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la I Mahakama ya Mwanzo Inonelwa Wilaya ya Misungwi. Kifo chake kilichotokea mnamo tarehe 07 Novemba, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mwanza Bw. Tutubi Mangazeni, marehemu Edmund aliajiriwa mnamo tarehe 25 Januari, 2021 katika Kada ya Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la II.

Baada ya kuajiriwa alipangiwa Kituo chake cha kwanza cha kazi huko Mahakama ya Mwanzo Bwasi Wilaya ya Bunda Masjala Ndogo ya Musoma na baada ya hapo akahamishiwa Mahakama ya Mwanzo Inonelwa mpaka umauti ulipomfika

Marehemu Edmund aliajiriwa kwa sifa ya elimu ya Stashahada ya Sheria (Diploma in Law) kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA)

Marehemu Edmund anatarajiwa kuzikwa Tanga Mjini mtaa wa Kange tarehe 12 Novemba, 2026.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni