Ijumaa, 24 Machi 2017

MATUKIO KATIKA PICHA MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA.

    Jaji Mfawidhi wa Mahakama  Kuu  Kanda ya Mbeya, Mhe.  Noel Chocha akielezea  jinsi utekelezaji wa usikilizaji wa mashauri katika kanda  hiyo, wakati alipofanya mahojiano maalum.  
    Mwonekano  wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambalo liko katika  ukarabati mkubwa ikiwa ni mojawapo ya  utekelezaji wa Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama ya Tanzania.

      Afisa  Utumishi  wa  Mahakama  Kuu Kanda ya Mbeya, Bw. Rajabu  Singana (kulia) akiangalia jinsi ujenzi wa  mnara wa kuwekea matanki ya maji  katika  Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya unavyoendelea, kushoto ni Mkandarasi wa jengo hilo, Peter Mtaita wa Kampuni ya ‘Masasi Construction Company Limited’. Jengo  hilo  liko  kwenye  ukarabati mkubwa ikiwa ni mojawapo ya  utekelezaji wa Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama ya Tanzania. Jengo hilo lipo maeneo ya Forest ya Zamani ambapo ndipo zilipo ofisi za Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.


  Baadhi ya watu wakisoma bango  na kuaangalia jengo la Mahakama ya Watoto, iliyopo    karibu  na Hospitali  ya Rufaa ya Mbeya. Tukio hilo limefanyika jana tarehe 23.03. 2017.

     Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwa nje ya jengo la Mahakama ya Mwanzo ya Mwanjelwa wakisubiri utaratibu wa mashauri mbalimbali. Watu hao walikuwa wakisuburi taratibu hizo jana tarehe   23. 03. 2017.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni