Jumapili, 21 Mei 2017

MAJAJI NA MAHAKIMU WATAKIWA KUFUATA MAADILI YA UHAKIMU NA UTUMISHI WA UMMA WAKATI WA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Beatrice Mutungi akifungua kikao cha Mahakimu wa Kanda ya Dar es salaam kilichohusu umuhimu wa maadili ya uhakimu na utumishi wa umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi  wa ofisi  ndogo ya Bunge uliopo jijini
Dar es Salaam.

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akizungumza na baadhi ya Mahakimu mbalimbali  wa Kanda ya Dares Salaam kuhusu umuhimu wa maadili  na  Utumishi wa Umma katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa ofisi  ndogo ya Bunge uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna wa kutoka Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji Amon Nsekela na kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Beatrice Mutungi.

Kamishna kutoka Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji Amon Nsekela akisisitiza jambo kuhusu umuhimu wa maadili ya Uhakimu na Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi mdogo wa Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa mahakimu wa Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika kikao kilichohusu umuhimu wa maadili  na  Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi  wa ofisi  ndogo ya Bunge uliopo jijini Dar es Salaam. Kanda ya Dar es salaam inahusisha mikoa ya Morogoro na Pwani.


Baadhi ya viongozi wa meza kuu wakifuatilia  mada ya Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji  Ilvin Mugeta (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichohusu umuhimu wa maadili  na  Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi  wa ofisi ndogo ya Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.


  Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, akitoa mada kuhusu maadili ya kazi ya Uhakimu wakati wa kikao kilichohusu umuhimu wa maadili  na  Utumishi wa Umma kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi mdogo wa Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.


Na Magreth Kinabo
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali, amewataka Majaji na Mahakimu kuzingatia maadili ya   Uhakimu na Utumishi wa Umma na kutenda haki kwa wakati wanapotimiza majukumu yao.

Aidha, Jaji huyo alisema Majaji na mahakimu wanaptimiza majukumu yao wanapaswa kuzingatia kanuni za utendaji wao na za utumishi wa umma hatua ambayo itawafanya kukidhi matakwa ya wananchi wanaowahudumia.

Kauli hiyo, imetolewa na Mhe. Jaji huyo   wakati akizungumza na baadhi ya Majaji na Mahakimu  mbalimbali katika kikao  kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi mndogo wa Bunge uliopo jijini Dar es Salaam.

“Suala la maadili lilianza tangu enzi za kale, jamii ilikuwa inajiwekea maadili, uwepo wa maadili ni heshima na utii, tabia ya uaminifu, uwajibikaji na kufuata  utaratibu kila unapotekeleza kazi,” alisisitiza Mhe. Jaji Kiongozi huku akisema masuala yalizishazungumziwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa, akiwemo Baba wa Taifa mwaka  Machi 15, mwaka 1984 na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Novemba 27, mwaka 2011.

Aliongeza kuwa suala la maadili ni muhimu katika kupambana na rushwa, pia linafanya Jaji na Hakimu awe na tabia njema mbele ya jamii, hivyo kazi hizo zinahitaji uadilifu na mtu mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Beatrice Mutungi akifungua kikao hicho, alisema kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili changamoto za kada hizo na kubadilishana uzoefu wakati wa kutatua changamoto hizo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na baadhi ya viongozi mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania.
 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni