Jumatatu, 16 Oktoba 2017

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA YAKUTANA NA WADAU WAKE KUBAINI MAENEO YA VIPAUMBELE KATIKA UPATIKANAJI WA HAKI

Naibu Katibu Mkuu-Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanji (aliyesimama) akifungua kikao cha Mahakama na Wadau wake ili kujadili na kubaini kwa pamoja maeneo ya Vipaumbele yatakayofanyiwa utafiti na maboresho ili hatimaye yasaidie kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati, akifungua kikao hicho kilichofanyika mapema Oktoba 16 katika ukumbi wa Mikutano wa Mahakama Kuu Mhe. Mpanji amewataka Wadau hao kubainisha maeneo hayo ili upatikanaji wa haki kwa wananchi uwe wa muda mfupi.
Baadhi ya Wadau wakiwa katika kikao hicho kilichoshirikisha Wawakilishi kutoka, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, RITA, Magereza, nk
Wadau wakiwa katika kikao hicho ambacho kwa pamoja na Mahakama watamaliza kikao hicho kwa kuwa maazimio ambayo yataorodhosha maeneo hayo ya kipaumbele.
Naibu Msajili Mwandamizi-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya akiongea na Wadau wa kikao hicho (hawapo pichani) katika maelezo yake kwa Wadau hao Mhe. Nkya amewaeleza juu ya maboresho mbalimbali yanayofanyika kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama lengo likiwa ni kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. 

Wakiwa katika picha ya pamoja. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)  


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni